Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya rekodi, ufundi wa Gamondi

GAMONDI Pict

Muktasari:

  • Gamondi alitua Juni 24,2023 kwa mara ya kwanza akija kuifundisha Yanga, akichukua nafasi ya Mtunisia Nasreddine Nabi ambaye aliachana na klabu hiyo kufuatia mkataba wake kumalizika, na mabingwa hao kumchukua Muargentina huyo.

ANAYEJUA anajua tu. Haya ndio maneno unayoweza kuyatumia kwa kocha Miguel Gamondi ambaye ameendelea kuweka alama za ubora akiwa kwenye ajira tatu tofauti nchini huku akiibua ubabe mpya kwa kikosi cha Taifa Stars.

Gamondi alitua Juni 24,2023 kwa mara ya kwanza akija kuifundisha Yanga, akichukua nafasi ya Mtunisia Nasreddine Nabi ambaye aliachana na klabu hiyo kufuatia mkataba wake kumalizika, na mabingwa hao kumchukua Muargentina huyo.

Alidumu Yanga kwa msimu mmoja akiipa mafanikio, huku ikiendelea kutamba na mataji ya ndani huku akiifikisha Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilipotolewa kwa mikwaju ya penalti na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kabla ya msimu uliofuata kusitishiwa mkataba kwa makubaliano maalum na uongozi wa klabu hiyo.

Baada ya kuondoka Yanga, Gamondi alirejea tena nchini Julai 3, 2025 akija kuifundisha Singida Black Stars huko nako akawapa ubingwa wa Kombe la Kagame Novemba 16, 2025 huku pia akiipeleka hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo mpya.

Mafanikio hayo yakamsogeza Gamondi akivutwa kuifundisha Taifa Stars kwa muda akichukua mikoba ya Hemed Suleiman ‘Morocco’, ambapo Fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Morocco zikawa ndiyo kipimo chake kikubwa.

GAMO 01

USHINDI MGUMU

Gamondi akiwa na Stars, ushindi mgumu uliomshinda ni kuipa ushindi wa kwanza timu hiyo ambapo bado iliendelea kusubiri kuona inashinda mechi yoyote, ikipata sare mbili na kupoteza moja kwenye mechi zake tatu za makundi ikipambana na timu za Tunisia, Nigeria na Uganda.


REKODI YA KUFUZU

Hata hivyo akaweka alama kubwa akiwa na Stars baada ya kufuzu hatua ya 16 akikata tiketi kama ‘best loser’ kutokana na sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia, akienda hatua inayofuata na Waarabu hao pamoja na Nigeria, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu hatua ya makundi tangu ianze kushiriki fainali hizo.

GAMO 02

MABADILIKO KIKOSI

Gamondi alifanya mabadiliko machache kwenye kikosi hicho ambapo hatua iliyoshtua ni kumweka nje beki mkongwe Shomari Kapombe kuanzia mchezo wa pili, akimpa nafasi Haji Mnoga aliyecheza mechi zote tatu za mwisho kwenye fainali hizo.

Mbali na Mnoga, Gamondi pia alifanya mapinduzi mengine akimrudisha benchi Dickson Job kisha kuanza kumtumia muda mchache, nafasi yake ikichukuliwa na Bakari Mwamnyeto aliyeonyesha kiwango bora.

Hata hivyo Gamondi hakumtupa Job, kwani kwenye mechi ngumu zilizohitaji ulinzi zaidi alimrudisha ndani akianza na mabeki watatu wa kati akiwemo, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ na Bakari Mwamnyeto, mabeki wote hawa aliwahi kufanya nao kazi Yanga.

GAMO 03

MIFUMO BALAA

Gamondi aliwapa kazi kubwa Nigeria, Tunisia na Morocco kutokana na mifumo yake migumu ya kulinda huku akishambulia kwa hesabu, hatua iliyowaongezea ubora Taifa Stars kwenye mechi hizo tatu ngumu.

Alipokutana na Nigeria, Gamondi aliwabana akitumia mfumo wa 4-2-3-1 huku ukuta wake uliokuwa na kipa Zuber Foba, mabeki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Bacca, Mwamnyeto na Kapombe ukifanya kazi bora ya kumzima mshambuliaji hatari Victor Osimhen licha ya kupoteza kwa mabao 2-1.

Gamondi alibadilika tena akatumia mfumo wa 4-5-1 alipokutana na Uganda, ambapo iliwapa wakati mgumu wapinzani wake, Stars wakitangulia kupata bao kabla ya kusawazishwa dakika za jioni na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo wa Tunisia, Gamondi alitumia mifumo miwili migumu akianza na 4-2-3-1 ambapo baada ya timu yake kutoka nyuma na kusawazisha, aliwabadilisha hesabu Waarabu hao akitumia mfumo wa 4-5-1 ambao uliwapa ugumu kukamilisha mashambulizi yao, mchezo huo ukimalizika kwa sare ya pili ya matokeo yale yale.

Mechi yenye presha kubwa ikawa ile dhidi ya Morocco ambapo wakati wengi wakiona Stars ingeteseka mbele ya wenyeji hao wa mashindano, Gamondi akaibuka na mfumo mwingine tofauti wa 3-4-1-2 ambao uliwatesa sana Waarabu hao.

Mfumo huo uliwapa wepesi Stars licha ya kucheza soka la mashambulizi ya kushtukiza, lakini walitengeneza nafasi hatari ambazo zilikosa umakini wa kuzitumia, wachezaji wakiwemo Simon Msuva na Feisal Salum.

Kwenye mchezo huo, ukuta wa Stars kwa mara ya kwanza ulianza na mabeki watatu wa kati Bacca, Mwamnyeto na Job ambao walionyesha kuelewana vizuri wakicheza kwa nidhamu kubwa, wakifanya kosa moja tu dakika ya 64 ambalo ndilo lilizalisha bao lililoamua mechi hiyo, likifungwa na mshambuliaji Diaz Brahimi anayeichezea Real Madrid ya Hispania.

GAMO 05

MASALANGA, FOBA GUMZO

Kuumia kwa kipa chaguo la kwanza Yakoub Seleman siku chache kabla ya kuanza kwa fainali hizo, presha ilikuwa kubwa juu ya nani ataibeba Stars golini, lakini Gamondi alianza kwa kumtumia Foba ambaye kwenye michezo dhidi ya Nigeria na Uganda alifanya kazi kubwa akionyesha ubora wa hali ya juu uwanjani akiisaidia timu hiyo kabla ya kuumia mazoezini.

Gamondi akafanya mabadiliko mengine akimpa nafasi Hussein Masalanga ambaye kuanzia mchezo dhidi ya Tunisia hadi ule wa Morocco alionyesha kiwango kikubwa akifanya kazi nzuri iliyoipa heshima Stars.

Makipa hao wawili hawatakuwa wageni tena kwenye kikosi cha Stars ambapo wameondoa presha kwa mashabiki kwamba imani waliyopewa na Gamondi itawafanya kuendelea kuaminiwa kwenye majukumu ya kikosi hicho.

GAMO 04

KAITEKA NCHI

Mechi hizo nne zimemtosha Gamondi kuwashawishi wadau wengi kuona kocha huyo anaweza kuipa mafanikio zaidi Stars, huku wakimsifu sana ili apewe muda zaidi wa kuifundisha timu hiyo wakivutiwa na namna timu ilivyobadilika uwanjani.