Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika huyu anawasikitisha Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo raia wa Denmark alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal baada ya kuibukia kutoka kwenye akademia ya wababe hao wa London Kaskazini, lakini kiwango chake kimekwenda kuwa tofauti huko kwingine alikokwenda.

MONACO, UFARANSA: STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Mika Biereth amepandisha thamani yake karibu mara 10 ya bei ambayo klabu hiyo ya Emirates ilimuuza na hivyo kuwafanya wajutie uamuzi huo, imeelezwa.

Fowadi huyo raia wa Denmark alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal baada ya kuibukia kutoka kwenye akademia ya wababe hao wa London Kaskazini, lakini kiwango chake kimekwenda kuwa tofauti huko kwingine alikokwenda.

Arsenal ilikubali kumuuza kwa Pauni 4 milioni kwenda Sturm Graz na baada ya Biereth kung'ara kwa mkopo msimu uliopita. Alicheza kwa miezi michache kabla ya kumchukuliwa na Monaco na iliipa klabu hiyo ya Austria mara tatu ya pesa ambazo ililipa wakati inamsajili kutoka Arsenal.

Biereth aliendelea kuwasha moto huko Monaco na mabao yake yameisaidia timu hiyo kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligue 1 na bado mechi moja, ambayo haiifanyi kuwa na presha yoyote.

Kiwango cha kufunga cha straika Biereth ndicho kinachowafanya kocha Mikel Arteta na mashabiki wa Arsenal kuwa kwenye masikitiko makubwa, kwanini walimruhusu kuondoka. Alifunga mabao 13 katika mechi 16 alizocheza kwenye ligi, huku akizidiwa na Ousmane Dembele wa PSG tu kwa kuwa na wastani mzuri wa bao kwa dakika.

Kwa mujibu wa L'Equipe, kuna klabu inamtaka straika huyo na ipo tayari kulipa Pauni 30 milioni ili kunasa huduma yake, ikiifanya Monaco kukuna kichwa juu ya ofa hiyo. Hata hivyo, Biereth si mchezaji pekee wa Monaco anayesakwa na timu nyingine, ikiwamo timu za Ligi Kuu England baada ya wengine Maghnes Akliouche na Eliesse Ben Seghir kuwindwa na vigogo ikiwamo Barcelona.

Gwiji wa Arsenal, Ian Wright alisema mshambuliaji Biereth angeweza kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho cha Emirates katika nyakati ambazo ilipoteza mastraika wake kutokana na kuwa majeruhi, aliposema: "Kusema ukweli angeweza kufanya kitu kwenye mpango wetu. Mika alipaswa kubaki kwenye timu yetu kwa ajili ya nyakati hizi."