Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kuchoma nyama ikibeba ubingwa

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Man United inahitaji ubingwa wa kombe hilo ili kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya mambo kwenda kombo kwenye ligi ya ndani. Fainali hiyo itapigwa Mei 21 huko Bilbao, Hispania na Man United inaripotiwa itakacha sherehe za kutembeza kombe mtaani kwenye basi la wazi badala yake watachoma tu nyama uwanjani Carrington kusherehekea.

MANCHESTER, ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Manchester United itaachana na mpango wa kutembeza kombe kwenye basi la wazi juu na badala yake itachoma tu nyama endapo kama itaichapa Tottenham Hotspur kwenye fainali ya Europa League.

Man United inahitaji ubingwa wa kombe hilo ili kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya mambo kwenda kombo kwenye ligi ya ndani. Fainali hiyo itapigwa Mei 21 huko Bilbao, Hispania na Man United inaripotiwa itakacha sherehe za kutembeza kombe mtaani kwenye basi la wazi badala yake watachoma tu nyama uwanjani Carrington kusherehekea.

Kikosi hicho kinachonolewa na Mreno, Ruben Amorim kinashika nafasi ya tano kutoka mkiani katika msimu wa Ligi Kuu England, lakini ipo nafasi moja juu ya Spurs, ambao ni wapinzani wao kwenye mechi hiyo ya fainali na watahitaji kushinda ili kukamatia tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini, kinachoripotiwa ni mabosi wa Man United au wapishi wa klabu hiyo wameripotiwa kuandaa mpango wa kuchoma nyama kama sehemu ya kusherehekea ushindi.

Baada ya mechi ya fainali, itakayopigwa Jumatano, Man United itamaliza msimu wao wa Ligi Kuu England kwa kukipiga na Aston Villa. Kisha itasafiri kwenda Asia kwenye mechi za kutafuta pesa na itafanya ziada ya michezo huko Kuala Lumpur na Hong Kong, Mei 28 na Mei 30.

Kwa maana hiyo, Man United italazimika kuendelea kusubiri kuona sherehe za kupitisha kombe mtaani na basi la wazi, kitu ambacho mara ya mwisho kilifanyika 2013, wakati iliponyakua taji la 20 la ligi chini ya Kocha Sir Alex Ferguson, ambaye aliongoza timu hiyo kwa miaka 27.