Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ivory Coast yatinga 32 bora kibabe ikiichapa Curacao

Muktasari:

  • Pepe mapema tu alianza kuitengeneza ramani ya Ivory Coast  ramani ya ushindi katika dakika ya saba akimalizia kwa mguu wa kushoto, krosi ya winga Yan Diomande.

Mabao mawili ya mshambuliaji Nicolas Pepe yametosha kuihakikishia ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Curacao, ikifuzu hatua ya 32 bora kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Pepe mapema tu alianza kuitengeneza ramani ya Ivory Coast  ramani ya ushindi katika dakika ya saba akimalizia kwa mguu wa kushoto, krosi ya winga Yan Diomande.

Baada ya bao hilo timu zote ziliongeza kasi ya kutengeneza mashambulizi lakini umakini wa kuzitumia ukakosekana na kufanya mechi hiyo kwenda muda wa mapumziko huku Ivory Coast ikiongoza kwa bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa Curacao kutafuta bao la kusawazisha lakini shida yao ikawa ileile ya kukosa utulivu karibu na lango la wapinzani wao huku kipa huyo wa Ivory Coast, Issa Fofana akiwa mwiba kwa kuokoa mashambulizi mawili mazuri.

Pepe tena akapiga bao la pili katika dakika ya 64 akimalizia pasi ya Ibrahim Sangare na kuifanya Ivory Coast kujihakishia ushindi kwenye mchezo huo.

Mabao hayo mawili ya Pepe yameirudisha Ivory Coast kwenye njia ya ushindi baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Ujerumani kwa mabao 2-1.

Ushindi huo wa Ivory Coast umeifanya ifikishe pointi sita na kuifanya imalize hatua ya makundi ikiwa kwenye nafasi ya pili katika kundi lao E,ikilingana  na vinara Ujerumani yenye pointi kama hizo baada ya jana kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Ecuador.

Ushindi huo wa Ecuador umeifanya ifikishe pointi nne na kuifanya ijihakikishie kufuzu hatua ya 32 bora  kupitia kundi la timu nane zenye matokeo bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu kwenye makundi yao (Best Losers) huku Curacao ikimaliza ya mwisho na pointi moja.

Ivory Coast imevunja mwiko kwa kutinga hatua hiyo ya 32 bora kwa mara ya kwanza baada ya kujaribu mara tatu bila mafanikio ikiungana na Morocco na  Afrika Kusini ambazo tayari zilishakata tiketi hiyo.