Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Canada yatinga 16 bora Sauzi ikishindwa kujishikilia Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Afrika Kusini imeshindwa kujishikilia kwani hadi inafika dakika ya 90, matokeo yalikuwa 0-0, muda wa nyongeza ndipo Stephen Eustáquio ambaye alipiga shuti kali baada ya walinzi wa Afrika Kusini kuokoa mpira vibaya, akafunga bao pekee dakika ya 90+2.

Los Angeles, Marekani: CANADA inakuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya dakika za jioni kuichapa Afrika Kusini bao 1-0.

Afrika Kusini imeshindwa kujishikilia kwani hadi inafika dakika ya 90, matokeo yalikuwa 0-0, muda wa nyongeza ndipo Stephen Eustáquio ambaye alipiga shuti kali baada ya walinzi wa Afrika Kusini kuokoa mpira vibaya, akafunga bao pekee dakika ya 90+2.

Sasa Canada itamsubiri mshindi kati ya Uholanzi na Morocco zitakazochuana kwenye hatua ya 32.

Canada ambayo ni muandaaji mwenza wa Kombe la Dunia 2026 kwa kushirikiana na Marekani na Mexico, ilikuwa bora kipindi cha dakika zote 90 licha ya umiliki wa mpira kwa asilimia 58 ulikuwa kwa Afrika Kusini, yenyewe ikiambulia 42, ilikosa tu bahati ya kufunga kabla ya kuitumia vizuri nafasi ya mwisho.

Katika mashambulizi, Canada ilitengeneza nafasi nne za kufunga, wakati Afrika Kusini ikiwa haina kitu, huku mashuti yaliyolenga lango, Canada inayo saba, Afrika Kusini moja pekee.

Licha ya Canada kushambulia lango la Afrika Kusini muda mwingi, Wasauzi walikuwa na nidhamu kubwa ya kuzuia.

Hata hivyo, Afrika Kusini nayo haikubaki nyuma muda wote, ilitengeneza nafasi na mara kadhaa ilisogea langoni mwa Canada lakini ilikosa utulivu kwenye eneo la kumalizia.

Canada kipindi cha pili ilifanya mabadiliko ya kumuingiza Alphonso Davies ambaye alikuwa hatari kwa mashambulizi kwenye eneo la kulia na kuipa uhai mkubwa timu hiyo.

Akizungumza baada ya kupoteza mechi hiyo, kipa wa Afrika Kusini, Ronwen Williams, amesema pamoja na kuondolewa, lakini wameonyesha kiwango bora.

Afrika Kusini inaaga mashindano ikiwa na kumbukumbu ya kumaliza nafasi ya pili katika Kundi A ikikusanya na pointi nne zilizoivusha kucheza mtoano, nyuma ya Mexico iliyomaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi tisa. Korea Kusini ilishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu huku Czech ikimaliza mkiani kwa pointi moja.

Canada nayo ilimaliza nafasi ya pili katika Kundi B kwa kukusanya pointi nne.