Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzize akomaa Ligi Kuu, vita mpya yaibuka

Muktasari:

  • Nyota huyo anayeitumikia Yanga kwa msimu wa tatu mfululizo sasa tangu alipopandishwa kutoka timu ya vijana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu, Nasreddine Nabi amewasha moto mkali msimu huu.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize ameiva. Angalia katika orodha ya wafungaji mabao wa Ligi Kuu Bara ndio utaelewa.

Nyota huyo anayeitumikia Yanga kwa msimu wa tatu mfululizo sasa tangu alipopandishwa kutoka timu ya vijana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu, Nasreddine Nabi amewasha moto mkali msimu huu.

Hii ni kutokana hadi sasa Mzize kuwa mchezaji pekee mzawa anaochuana na mapro wa kigeni katika mbio za kuwania Kiatu cha dhahabu cha Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, huku ligi hiyo ikisaliwa na mechi za raundi mbili tu kumalizika.

Nyota huyo wa kimataifa wa Tanzania, amefunga mabao 13 akilingana na mchezaji mwenzake, Prince Dube raia wa Zimbabwe, wakitanguliwa na kinara Jean Charles Ahoua wa Simba, lakini akiwaburuza mastaa wengine wa kigeni wanaomfuata nyuma yake katika orodha ya wafungaji hadi sasa akiwa ni mchezaji mzawa aliyewatoa jasho wageni.

Mzize ambaye huu ni msimu wa tatu kucheza Ligi Kuu Bara akipandishwa kutoka timu ya vijana ya Yanga, kwa sasa ana mabao 13, sawa na Mzimbabwe Prince Dube anayecheza pia Yanga.

Nyota huyo msimu huu kwake umekuwa bora zaidi kwani idadi hiyo ya mabao imekuwa mara mbili zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita 2023-2024 alipomaliza na mabao sita, huku ule wa kwanza 2022-2023 akifunga matano.

Mzize ndani ya kikosi cha Yanga, msimu huu ndiye mchezaji aliyecheza mechi zote za ligi hadi sasa ambazo ni 27 akitumika kwa dakika 1,678.

Katika chati hiyo ya ufungaji msimu huu, kinara ni Muivory Coast Jean Charles Ahoua wa Simba mwenye mabao 15, huku Leonel Ateba raia wa Cameroon anayecheza Simba akifunga mabao 12. Mghana Jonathan Sowah wa Singida Black Stars ana mabao 11 sawa na Mganda Steven Mukwala wa Simba.

Mkenya Elvis Rupia anayecheza Singida Black Stars, amefunga mabao 10, akifuatiwa na Muivory Coast Pacome Zouzoua wa Yanga na Gibril Sillah raia wa Gambia anayecheza Azam ambao kila mmoja amefunga mabao tisa.

Mzawa mwingine unakuja kumkuta Paul Peter wa Dodoma Jiji mwenye mabao manane sawa na Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso anayecheza Yanga.

Kitendo cha Mzize kuwa katikati ya wageni kwenye chati hiyo, kinamfanya mshambuliaji kutolewa macho zaidi kama ndiye mkombozi wa wazawa huku zikibaki mechi tatu kwa Yanga kucheza dhidi ya Simba, Tanzania Prisons na Dodoma Jiji.

Wakati hali ikiwa hivyo kwenye ufungaji, wazawa wameendelea kukimbizwa tena upande wa takwimu za clean sheet kwani hivi sasa kinara ni Moussa Camara raia wa Guinea anayecheza Simba akiwa nazo 16, akifuatiwa na Djigui Diarra wa Yanga mwenye 15. Diarra ni raia wa Mali ambapo anaendelea kupambana kuwania Tuzo ya Kipa Bora aliyoipoteza msimu uliopita na kuchukuliwa na Mkongomani, Ley Matampi aliyekuwa Coastal Union.

Wakati Matampi anabeba tuzo hiyo, alikuwa na clean sheet 15 wakati Diarra akiwa na 14, msimu huu Diarra amevunja rekodi yake kwa kufikisha clean sheet 15. Kumbuka kipa huyo huu ukiwa ni msimu wa nne anaitumikia Yanga, tayari anatuzo mbili za kipa bora wa Ligi Kuu Bara alizochukua 2021-2022 na 2022-2023.

Chini ya Diarra, kuna mzawa Patrick Munthari anayecheza Mashujaa akiwa na clean sheet 11. Huku kidogo kumechangamka kwani wazawa kidogo wanapambana wawili wakiingia tano bora. Mwingine ni Yona Amosi wa Pamba Jiji mwenye 10.

Feisal Salum 'Fei Toto', ni mzawa anayekimbiza katika asisti akiwa nazo 12, ndiye kinara wa jumla mpaka sasa akifuatiwa na Pacome Zouzoua na Max Nzengeli wenye tisa kila mmoja wakiitumikia Yanga. Prince Dube ana nane, Stephane Aziz (Yanga), Jean Cherles Ahoua (Simba) na Muivory Coast Josephat Bada (Singida BS) kila mmoja anazo saba, kisha mzawa Salum Kihimbwa wa Fountain Gate anazo tano sawa na Mkongomani wa Simba, Ellie Mpanzu.

Kuhusu suala la kufunga, Mzize aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Kufunga ndio kazi ya mfungaji, nami naona raha kila ninapoisaidia timu, kwa ishu ya Mfungaji Bora siwezi kuzungumzia, lakini kiu ni kuona Yanga inatetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.”

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 73 baada ya mechi 27, ikifuatiwa kwa karibu na Simba yenye 69 ikicheza mechi 26 na zenyewe zina kiporo chao cha Dabi ya Kariakoo ili kutangaza bingwa wa msimu huu, lakini mabao 71 iliyofunga Yanga imeifanya ifikie idadi ya msimu uliopita ilipotetea taji kwa msimu wa tatu mfululizo.