Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bunge lapokea pongezi za Simba, Yanga katika viwango vya ubora

Muktasari:

  • Waziri Profesa Kabudi amesema timu hizo na nyingine za Tanzania katika michezo mbalimbali zimeiweka nchi katika ramani ya juu ya michezo

 Serikali imezimwagia sifa klabu za Simba na Yanga kwa kuendelea kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa barani Afrika.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi ambaye amesema juhudi za klabu hivyo zimewezesha ligi ya Tanzania kushika nafasi ya nne kwa ubora Afrika.

Profesa Kabudi ametoa kauli hiyo Bungeni leo Jumatano alipokuwa akisoma Hotuba ya Mapato na Makadirio ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025/26 ambapo ameomba Sh519.66bilioni.

"Pongezi za kipekee ziende kwa klabu ya Simba kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ni imani yetu kwa mara ya kwanza klabu hii itakwenda kulitwaa kombe hili, Simba nguvu moja," amesema Profesa Kabudi.

Waziri amesema jitihada zote hizo zinatokana na hamasa ya 'Goli la Mama' ambayo ni ubunifu na mchango mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa karibu zaidi na wanamichezo.

Aidha, Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 Tanzania iliendelea kufanya vizuri katika michezo mbalimbali hata kupelekea timu za vijana, Taifa Stars na mchezo wa kriketi kuweka rekodi ya kufuzu kwa hatua za juu.