Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa Sugar haijajifunza kwa makosa

Muktasari:

  • Kikanuni, kama itamaliza katika nafasi hiyo, itatakiwa kucheza hatua ya mchujo ili kupambania nafasi ya kubaki kwenye ligi na mwanzoni itacheza na timu iliyo nafasi ya 13.

UKIANGALIA msimamo wa Ligi Kuu ya NBC hivi sasa, utaona Mtibwa Sugar ipo katika nafasi ya 14 ambayo ni ya tatu katika timu zilizo chini kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo.

Kikanuni, kama itamaliza katika nafasi hiyo, itatakiwa kucheza hatua ya mchujo ili kupambania nafasi ya kubaki kwenye ligi na mwanzoni itacheza na timu iliyo nafasi ya 13.

Hata hivyo, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwa Mtibwa Sugar ikiwa haitofanya vizuri katika michezo miwili inayofuata ambayo itakabiliana na Tanzania Prisons na Namungo FC ambazo zote itacheza ugenini.

Mchezo mgumu zaidi ni dhidi ya Tanzania Prisons ambao ndio unafuata kwa sababu utofauti wa pointi baina ya timu hizo mbili ni pointi moja tu na Mtibwa ina pointi 26 na Maafande wa Prisons wana pointi 25.

Hii inamaanisha kama Mtibwa itapoteza mchezo huo, itashuka hadi nafasi ya 15 ambayo timu inayomaliza msimu ikiwa hapo, inashuka daraja moja kwa moja ikiungana na timu iliyopo nafasi ya 16 kwenye msimamo.

Kinachotusikitisha hapa kijiweni ni hii Mtibwa Sugar msimu uliopita tu ilikuwa Ligi ya Championship baada ya kushuka daraja katika msimu wa 2023/2024.

Tulitegemea baada ya kupitia mateso ya kushuka daraja, ingerudi kwa nguvu kubwa Ligi Kuu ili isirudi tena shimoni lakini mambo yamekuwa tofauti na hali inaonekana kuwa mbaya kwa upande wake.

Jambo la kushangaza zaidi, mzunguko wa pili ambao kikawaida ndio huamua hali ya mambo kwenye msimamo wa ligi, ndio ambao Mtibwa Sugar imeangusha pointi nyingi zaidi kulinganisha na mzunguko wa kwanza.

Katika mechi 13 ilizocheza hadi sasa katika mzunguko wa pili, imepata pointi sita tu huku ikipoteza pointi 33. Inashangaza kiukweli.