Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uzao wa Wema Sepetu kama kina Mariah Carey, J. Lo

Muktasari:

  • Hata hivyo, Wema si staa wa pekee aliyejaliwa mtoto wa kwanza akiwa ameshavuka umri wa miaka 35, kina Mariah Carey, Jennifer Lopez, Madonna na wengineo wengi walikuwa sehemu ya kundi hilo.

IMEKUWA habari njema na kubwa kwa mashabiki wengi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, 35, baada ya kujaliwa mtoto wake wa kwanza baada ya mapambano ya muda mrefu kama alivyowahi kuelezea.

Hata hivyo, Wema si staa wa pekee aliyejaliwa mtoto wa kwanza akiwa ameshavuka umri wa miaka 35, kina Mariah Carey, Jennifer Lopez, Madonna na wengineo wengi walikuwa sehemu ya kundi hilo.

Makala haya yanakuletea orodha ya wasanii wa kimataifa kutokea kiwanda cha muziki, filamu na mitindo ambao walipata watoto wao wa kwanza katika umri sawa na Wema Sepetu au zaidi ya hapo kama ifuatavyo.

1. Janet Jackson

Mwimbaji Janet Jackson, 60, aliwashangaza na kuwapa moyo watu wengi duniani alipomzaa mtoto wake wa kwanza, Eissa Al Mana akiwa na umri wa miaka 50!, safari yake iliwaonyesha wanawake wengi kuwa bado inawezekana kuwa mama hata katika umri mkubwa.

Janet ambaye ni ndugu na mwanamuziki Michael Jackson, alijifungua hapo Januari 3, 2017, wakati huo akiwa bado katika ndoa na mumewe wa zamani Wissam Al Mana, mfanyabiashara mkubwa wa Qatar.

Tetesi za Janet kuwa mjamzito zilianza Aprili 2016 baada ya kusitisha ziara yake ya muziki, Unbreakable World Tour ili kujitayarisha na uzazi. Kwa mujibu wa taarifa iliyoitoa kwa video, alisema yeye na mume wake walikuwa wanapanga kuanzisha familia, hivyo alilazimika kuahirisha ziara hiyo.


2. Madonna

Miezi miwili baada ya Madonna, 67, kutumia umri wa miaka 38 ndipo alipojaliwa mtoto wake kwanza, Lourdes hapo Oktoba 14, 1996, wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa na uhusiano na Carlos Leon.

Madonna, mkali wa kibao cha La Isla Bonita (1985), kupata mtoto ilikuwa furaha kubwa kwake hadi kuandika wimbo 'Little Star' unaopakana kwenye albamu yake, Ray of Light (1998) iliyoshinda Grammy.

Mtoto huyo wa Madonna kwa sasa ana umri wa miaka 30, kazi yake ni mitindo na amehusika kutangaza bidhaa za urembo za Rihanna, Savage x Fenty, huku akitokea kwenye kava za majarida makubwa kama Vogue na Vanity Fair.


3. Naomi Campbell

Mwanamitindo wa Uingereza, Naomi Campbell, 56, aliwashangaza mashabiki wengi alipotangaza kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza hapo Mei 2021, wakati huo akiwa na umri wa miaka 51.

Supermodel huyo, kufikia Juni 2023 akiwa na umri wa miaka 53, akatangaza kujaliwa mtoto mwingine, awamu hii akipata wa kiume baada ya awali kupata msichana.

Hata hivyo, Naomi Campbell aliliambia Jarida la Vogue alipata watoto hao kwa njia ya mama mbadala (surrogacy), yaani mwanamke mwingine alimbebea ujauzito, hivyo yeye anasalia kuwa mama wa kibaolojia.

4. Jennifer Lopez

Akiwa na umri wa miaka 38 ndipo mwanamuziki na muigizaji, Jennifer Lopez, 56, alijaliwa watoto wake wa kwanza ambao ni pacha, Max na Emme waliozaliwa hapo Februari 22, 2008.

Lopez aliyevuma na wimbo wake, I'm Into You (2011), alijaliwa pacha hao wakati huo bado alikuwa katika ndoa na mwanamuziki mwenzake, Marc Anthony ambaye ndoa yao ilidumu kwa takribani miaka 10.

Kwa sasa watoto ambao wametimiza umri wa miaka 18 wanajiandaa kwenda chuo, hatua ambayo Lopez amesema itamuacha na upweke mkubwa kwa sababu ameishi nao kwa kipindi chote.


5. Mariah Carey

Katika ndoa na mumewe wa zamani Nick Cannon, ndipo mwimbaji Mariah Carey alijaliwa watoto wake pacha hapo Aprili 30, 2011 ukiwa na uzao wake wa kwanza wakati huo akiwa na umri wa miaka 42.

Mkali huyo wa ngoma, Always Be My Baby (1995), alisema kabla ya kupata pacha hao alilamizika kupata matibabu fulani ya uzazi baada ya ujauzito wake wa kwanza kuharibika (miscarriage).

Katika kitabu chake kiitacho The Meaning of Mariah Carey (2020), mwimbaji huyo alieleza alitaka watoto wake wote herufi za mwanzo za majina yao zifanane ndipo akawaita Monroe na Morocco.