Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gattuso apendekeza Ligi Kuu Italia isimame kwa muda

GATTUSO Pict

Muktasari:

  • Azzurri itakutana na Ireland Kaskazini katika mechi ya nusu fainali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, Machi 26, 2026 kwenye uwanja wa nyumbani, na mshindi atacheza mechi ya fainali dhidi ya mshindi kati ya Wales na Bosnia & Herzegovina.

Kocha wa timu ya taifa ya Italia, Gennaro Gattuso, ameomba mechi za Serie A zilizopangwa kabla ya mechi za mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, ziahirishwe ili kutoa muda kwa kikosi hicho maarufu Azzurri kuikabili Ireland Kaskazini.

Azzurri itakutana na Ireland Kaskazini katika mechi ya nusu fainali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, Machi 26, 2026 kwenye uwanja wa nyumbani, na mshindi atacheza mechi ya fainali dhidi ya mshindi kati ya Wales na Bosnia & Herzegovina.

Kwa sasa hakuna mapumziko ya kimataifa hadi Machi 2026, jambo linalomaanisha kuwa Gattuso atakuwa na muda mdogo wa kujiandaa kwa mechi hiyo. 

Shirikisho la Soka la Italia linatarajia kupata nafasi Februari 2026, kwa ajili ya maandalizi katika kituo cha Coverciano, lakini inaweza kuwa kazi ngumu kutokana na ratiba nzima ya mechi za Serie A na Ulaya.

GATT 01

Kutokana na ufinyu huo wa muda, Gattuso amependekeza chaguo lingine ambalo anaamini litamsaidia kujiandaa kwa mechi hiyo muhimu, ambayo imebaki kama silaha ya mwisho itakayoipeleka Italia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

“Nimezungumza na baadhi ya wenzangu. Nimesikia kwamba nchini Uturuki, huenda ligi ikasimama kwa siku tatu. Natumai na sisi hapa Italia tunaweza kufanya hivyo, ili kuwa na nafasi ya kujiandaa kabla ya kucheza katika mashindano ya Ulaya na labda kupata siku tatu nyingine zaidi,” Gatuso ameiambia RAI.

“Tunahitaji kufikiria tu kuhusu mechi ya kwanza. Kisha Bosnia na Wales ni timu tofauti, zenye mitindo tofauti ya kucheza, mazingira tofauti, lakini kipaumbele ni Ireland Kaskazini, hivyo tunaweza kuanza kuzingatia Bosnia na Wales baadaye,” Gattuso ameendelea.

GATT 02
GATT 02

Kocha huyo wa timu ya taifa ya Italia, tayari alikuwa ameipongeza Ireland Kaskazini kwa mfumo wake wa kutumia nguvu kwenye mechi zake na akasisitiza Azzurri lazima ijitayarishe kwa mechi ngumu.

“Ireland Kaskazini ni timu yenye nguvu za kimwili, wanapenda kucheza mipira ya pili, na hakika tutahitaji mchezo mzuri, lakini tunaweza kushughulikia suala hilo kwa kufanya maandalizi mazuri,” ameongeza.

“Tuchukulie tu mchezo wa kwanza. Tunajua ni timu gani Wales na Bosnia. Hakika mazingira nchini Wales ni magumu, wanashinikiza kwa nguvu, kama walivyozoea. Bosnia ni vivyo hivyo, viwanja hivyo vinaweza kumfanya mtu yeyote kushindwa, lakini hauna maana kuzizungumzia sasa. Tuna nusu fainali, tuendelee kisha tutaona mpinzani na jinsi ya kumkabiliana naye.”

Mechi ya nusu fainali kati ya Italia dhidi ya Ireland Kaskazini huenda ikachezwa kwenye New Balance Arena huko Bergamo, uwanja unaotumiwa na klabu ya Atalanta inayoshiriki Ligi Kuu ya Serie A.

Italia itacheza mechi za mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, baada ya kushindwa kufuzu moja kwa moja kupitia mechi za makundi ukanda wa Ulaya. 

Katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, timu zinapangwa katika makundi na timu zilizoongoza moja au mbili zimefuzu moja kwa moja, huku zile zilizoshika nafasi za pili au nafasi maalumu zikipangiwa mechi ya mchujo ili kupata nafasi ya kucheza fainali.

Katika msimamo wa Kundi I, Italia ilimaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi 18, ikitanguliwa na Norway iliyokuwa na pointi 22 ambazo ziliipa nafasi ya kufuzu moja kwa moja, hivyo Azzuri inapaswa kujitafuta kwenye m,echi za mchujo ili kutimiza lengo la kufuzu Kombe la Dunia 2026.