Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘The Special One’ atajwa kuwa mrithi wa Arbeloa Real Madrid!

MOURINHO Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa, Mourinho sasa anaangaliwa kama mrithi wa Alvaro Arbeloa katika wakati huu ambao rais wa klabu Florentino Perez pamoja na viongozi wengine wakitathmini mustakabali wa benchi la ufundi baada ya kutolewa kwao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bayern Munich wiki iliyopita.

BENFICA, URENO: KOCHA wa Benfica, Jose Mourinho ‘The Special One’ ameripotiwa kuhusishwa na kurejea Real Madrid kuelekea msimu ujao kwani tayari mabosi wa timu hiyo wameanza mazungumzo na wawakilishi wake.

Kocha huyo mkongwe wa kimataifa wa Ureno kwa sasa anapambana kutwaa ubingwa wa ligi akiwa na Benfica, baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Madrid, katika hatua ya 16 bora.

Kwa mujibu wa taarifa, Mourinho sasa anaangaliwa kama mrithi wa Alvaro Arbeloa katika wakati huu ambao rais wa klabu Florentino Perez pamoja na viongozi wengine wakitathmini mustakabali wa benchi la ufundi baada ya kutolewa kwao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bayern Munich wiki iliyopita.

Kipigo hicho kimekuja sambamba na kushuka kwa kiwango kwenye ligi na Madrid imepata pointi moja tu katika mechi zao mbili zilizopita dhidi ya RCD Mallorca na Girona FC.

Matokeo hayo yamewaacha wakiwa nyuma kwa pointi tisa dhidi ya wapinzani wao FC Barcelona waliopo kileleni, hali inayoongeza presha juu ya mustakabali wa muda mrefu wa kocha Arbeloa katika kikosi chao.

Inaripotiwa Mourinho amewekwa juu katika orodha ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi hiyo, ikiwa Arbeloa  ataondolewa.

 Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63, ambaye aliwahi kuinoa Manchester United, anaelezwa yuko tayari kurejea licha ya sintofahamu zilizotokea wakati alipokuwa akiifundisha klabu hiyo na kuondoka  mwaka 2013.

“The Special One” aliwahi kuinoa Real Madrid kati ya mwaka 2010 hadi 2013, akitwaa mataji ya La Liga na Copa del Rey kabla ya kuondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili na kurejea Chelsea.

Licha ya kuwa bado ana mkataba na Benfica, Mourinho anaelezwa kuwa tayari kuchukua dili hilo ingawa pia kuna ripoti zinazodai kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, ametajwa kwenye orodha hiyo licha ya yeye mwenyewe kukanusha taarifa hizo.