Marioo na Paula watarajiwa kupata mtoto 

Muktasari:

  • Paula ni mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja na mzalishaji muziki P Funk Majani. Kabla ya kuwa na Marioo aliwahi kuwa kwenye uhusiano ya kimapenzi na mwanamuziki Raymond Mwakyusa maarufu kama Rayvanny. Ambapo baada ya kuachana msanii huyo alirudiana na mzazi mwenziye Faima Msengi maarufu kama Fahyma.

Baada ya kuzuka tetesi kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Paula Kajala ana ujauzito wa mwanamuziki Marioo, hatimaye wawili hao wamethibitisha kuwa wanatarajia kupata mtoto.

Kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram wamechapisha video ikimuonyesha Paula akiwa na ujauzito, huku ikiambatana na ujumbe ulioeleza kuwa, wanatarajia kuongeza mwanafamilia mpya hivi karibuni.

Paula ni mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja na mzalishaji muziki P Funk Majani. Kabla ya kuwa na Marioo aliwahi kuwa kwenye uhusiano ya kimapenzi na mwanamuziki Raymond Mwakyusa maarufu kama Rayvanny. Ambapo baada ya kuachana msanii huyo alirudiana na mzazi mwenziye Faima Msengi maarufu kama Fahyma. 

Utakumbuka kuwa tetesi za Paula kuwa na ujauzito zilianza mwishoni mwaka jana baada ya kuonekana akiwa ameongezeka mwili na zilizidi baada ya kuwa anavaa nguo kubwa za kumwaga kama alivyofanya kwenye sherehe ya Haji Manara, alipokuwa akimvisha pete ya uchumba Zaylissa.