Kipande cha mlango kilichookoa maisha ya Rose wa Titanic chauzwa 

Muktasari:

  • Mauzo hayo yamefanyika katika mnada wa vifaa na mavazi wa Heritage Auctions Hollywood huku wauzaji wakiweka wazi kuwa kipande hicho kilichotumika kwenye filamu hiyo ni cha mabaki yaliookolewa kutoka kwenye ajali ya Titanic mwaka 1912.

Kipande cha mlango wa mbao kilichookoa maisha ya Rose wa filamu ya Titanic kimeuzwa kwa dola 718,750 ikiwa ni zaidi ya Sh 1.8 bilioni.

Mauzo hayo yamefanyika katika mnada wa vifaa na mavazi wa Heritage Auctions Hollywood huku wauzaji wakiweka wazi kuwa kipande hicho kilichotumika kwenye filamu hiyo ni cha mabaki yaliookolewa kutoka kwenye ajali ya Titanic mwaka 1912.


                     

Vifaa vingine vilivyouzwa katika mnada huo ni pamoja na Mjeledi wa Harrison Ford kutoka kwenye filamu ya "Indiana Jones and the Temple of Doom", ambayo iliuzwa kwa Dola 525,000, Suti ya Spiderman inayovaliwa na Toby Maguire iliuzwa kwa Dola 125,000 na bidhaa nyingine.

Filamu ya Titanic ilitoka rasmi Disemba 19, 1997, ikioongozwa na James Cameron ambapo ilitumia bajeti ya Dola 200 milioni na kufanikiwa kuuzwa na kupata faida ya zaidi ya Dola 2.26 bilioni.