Mwalimu adaiwa kumbaka mwanafunzi nyumbani kwake

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nikodemus Katembo akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo katika picha hiyo. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Mwalimu Masasi ashikiliwa na Polisi kwa kosa la kubaka Mwanafunzi (14) wa darasa la saba nyumbani kwake.

Mtwara. Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mtu mmoja (23) mkazi wa kijiji cha Mkalapa kata ya Chikundi ambaye ni mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Mkalapa kwa tuhuma za kumbaka binti (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatno Septemba 20,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nikodemus Katembo amesema kuwa Septemba 18  katika Kijiji cha Mkalapa, Kata ya Chikundi, Wilaya ya Masasi mkoani wa Mtwara mtuhumiwa huyo alikuwa ni mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Mkalapa.

Amesema kuwa inasemekana kuwa mwalimu huyo alimwita binti huyo nyumbani kwake baada ya kuingia ndani alimkamata na kumziba mdomo ili asipige kelele kisha akaanza kumbaka.

Ambapo mzazi wa binti huyo alipata taarifa za siri kuwa mwanaye ameingia ambapo alibainika kuingiliwa na hali yake ya kiafya inaendelea vizuri ambapo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Nitoe rai kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Pili kukomesha kabisha vitendo hivi vya ukatili dhidi ya watoto.

Aidha jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kuhakiksha kuwa Mkoa wa Mtwara unaendelea kuwa salama.