Mafuriko Jangwani, mwendokasi yasitisha huduma

Muktasari:

  • Aidha, huduma ya usafiri wa mabasi ya Dart inaendelea kutolewa eneo la katikati ya jiji kwa njia ya Muhimbili na Gerezani na ile ya Kimara hadi Moroco.

Dar es Salaam. Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) umeifunga Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani asubuhi ya leo Alhamisi Mei 9, 2024 kutokana na mafuriko ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini ikiwemo jijini Dar es Salaam.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na  Dart imesema kutokana na kufungwa kwa eneo hilo,  mabasi kwa njia za Kimara hadi Kivukoni na Gerezani yanaishia Magomeni Mapipa.

Aidha, huduma ya usafiri wa mabasi ya Dart inaendelea kutolewa eneo la katikati ya jiji kwa njia ya Muhimbili na Gerezani na ile ya Kimara hadi Moroco.

Pia, huduma za mabasi katika mfumo wa Dart zinaendelea kama kawaida katika njia Mlishi ya Kimara hadi Mbezi, Kimara hadi Kibaha na Kimara hadi Mlonganzila.

Si mara ya kwanza kwa eneo hilo kufungwa pindi mvua kubwa zinaponyesha. Imekuwa kawaida kila mvua zinaponyesha maji hujaa barabarani na wakala huyo kusitisha huduma.