Ahadi ya Serikali kwa wakulima wa ndizi

Ahadi ya Serikali kwa wakulima wa ndizi

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imeweka mikakati ya kukuza kilimo cha ndizi kuwa kilimo cha biashara ili kuongeza uzalishaji pamoja na kukuza soko la kimataifa ili kuongeza pato la Taifa.

  



Moshi. Serikali ya Tanzania imeweka mikakati ya kukuza kilimo cha ndizi kuwa kilimo cha biashara ili kuongeza uzalishaji pamoja na kukuza soko la kimataifa ili kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Agosti 14, 2021 na waziri wa kilimo Tanzania, Profesa Adolf Mkenda wakati alipotembelea mashamba ya wawekezaji ya maua, ndizi na makademia. Aliambatana na kamati ya bunge ya kilimo ,mifugo na maji.

Amesema zipo baadhi ya nchi zimenufaika na kilimo hicho hivyo kikiendelezwa hapa Tanzania wakulima watapa fursa ya kuuza zao hilo kwenye masoko ya kimataifa.

 "Mwisho wa mwezi wa Novemba mwaka huu tutafanya mkutano na wadau wa ndizi ikiwa ni pamoja na wanasayansi ,watafiti ,wataalamu wa masoko pamoja na kampuni za kusafirisha na kununua ndizi hapa nchni,"amesema na kuongeza

"Lengo ili tuangalie namna ya kuendeleza kilimo cha ndizi hapa nchi  ili tuongeze uzalishaji kwa ajili ya chakula chetu na kwaajili ya kuuza kwenye masoko ya Kimataifa ,zipo nchi zinatengeneza sana fedha nyingi kwa sababu ya kuuza ndizi na hii ni fursa kwa nchi yetu,"amesema Profesa Mkenda.


Imeandikwa na

Janeth Joseph na Omben Daniel