Mwili wa O.J. Simpson utachomwa moto kukwepa uchunguzi

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya Orange County Register imeripoti kuwa baada ya taratibu zote kufanyika mwili huo utachomwa moto kwa sababu ya kupoteza ushahidi wa ubongo wake kuchukuliwa na kutumika kwenye kituo maalumu cha utafiti wa masuala ya ubongo 'CTE' nchini humo.

Mwili wa aliyekuwa mwanamichezo wa zamani ambaye pia alikuwa mwigizaji kutoka nchini Marekani O. J. Simpson utachomwa moto baada ya kukamilika taratibu za kumhifadhi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Orange County Register imeripoti kuwa baada ya taratibu zote kufanyika mwili huo utachomwa moto kwa sababu ya kupoteza ushahidi wa ubongo wake kuchukuliwa na kutumika kwenye kituo maalumu cha utafiti wa masuala ya ubongo 'CTE' nchini humo.

Uchunguzi huo unakuja baada ya mwigizaji huyo kuwahi kushutumiwa kufanya mauaji mara mbili.

Kabla ya kifo chake Simpson aliwahi kuzungumzia kuhusu ugonjwa wake wa wasiwasi unaotokana na mishtuko mingi aliyowahi kuipata wakati wa mechi za American Football.

O.J. Simpson alifariki dunia wiki iliyopita kwa tatizo la saratani ya tezi dume iliyogundulika miezi miwili iliyopita.