Kanye West amtamani mke wa Obama

Muktasari:

  • Kupitia mahojiano yake na ‘The Download Podcast’ Kanye alipoulizwa swali kuwa ni mwanamke gani mwingine angependa kuwa naye akiachana na mpenzi wake Bianca ndipo akajibu anatamani kuwa na Michelle Obama.

Rapa Kanye West amefunguka kutamani kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, Michelle Obama.

Kupitia mahojiano yake na ‘The Download Podcast’ Kanye alipoulizwa swali kuwa ni mwanamke gani mwingine angependa kuwa naye akiachana na mpenzi wake Bianca ndipo akajibu anatamani kuwa na Michelle Obama.

Kanye kwa sasa yupo kwenye ndoa na mwanadada Bianca Censori ambaye amekuwa akizua gumzo katika mitandao ya kijamii kutokana na aina ya mavazi anayovaa.

Ikumbukwe kuwa wawili hao January mwaka 2023 walifunga ndoa baada ya Kanye kutalikiana na aliyekuwa mke wake na mzazi mwenzie Kim Kardashian.

Aidha Michelle na Obama walifunga ndoa Octoba 3, 1992. Na kufanikiwa kupata watoto wawili wa kike ambao ni Malia Ann aliyezaliwa (1998) na Natasha maarufu kama Sasha (2001).