Jina la Prince Harry latokea kwenye nyaraka za mahakamani , kesi ya Diddy

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya Mail Online, imeeleza kuwa kesi iliyohusisha jina la Prince Harry ni ile iliyofunguliwa Februari 26 huku Jones akidai kuwa uhusiano wa Diddy na Prince pamoja na nyota wengine ulimpa yeye na washirika wake uhalali wa kufanya matukio hayo.


Mapya yameibuka baada ya jina la Prince Harry ambaye ni mtoto wa Mfalme Charles III na Diana, kuonekana katika nyaraka za mahakama,kwenye kesi iliyowahi kufunguliwa na mtaarishaji wa muziki Rodney 'Lil Rod' Jones' dhidi ya P Diddy kuhusiana na madai ya $30M zaidi ya 76.4 Bilioni kama fidia kutokana na unyanyasaji wa kingono aliyowahi kufanyiwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Mail Online, imeeleza kuwa kesi iliyohusisha jina la Prince Harry ni ile iliyofunguliwa Februari 26 huku Jones akidai kuwa uhusiano wa Diddy na Prince pamoja na nyota wengine ulimpa yeye na washirika wake uhalali wa kufanya matukio hayo.

Licha ya Prince Harry kuwa ni miongoni mwa waliotajwa kwenye hati ya mahakama kwenye kesi inayomkabili Diddy, siyo mshtakiwa katika kesi hiyo na hajahusishwa na makosa yoyote.

Ikumbukwe kuwa Jones alimshutumu Diddy kwa unyanyasaji wa kijinsia, dawa za kulevya, na kupewa vitisho kati ya Septemba 2022 na Novemba 2023.

Kwa mujibu wa NBC, ilieleza kuwa Jones ambaye alitayarisha nyimbo tisa kwenye albamu ya Diddy ya 2023, Love, alisema wakati akifanya kazi ya utayarishaji wa albamu hiyo, alikuwa akiishi kwa Diddy na kusafiri naye hivyo wakati huo wote alikuwa akipitia unyanyasaji wa mara kwa mara.

Ikiwemo kupapaswa sehemu zake za siri, huku akikumbushia Februari 2023, aliamka akiwa mtupu huku akihisi kizunguzungu, hivyo anaamini Diddy alikuwa amemlewesha kwa dawa za kulevya.