Mjane alivyokuza kipato kupitia mpango wa kidigitali kutoka Yara Tanzania

“Misimu mitatu sasa nalima chini ya mpango wa kidigitali wa Yara na nimepata faida kubwa sana kwa sababu sasa hivi nalima kwa tija kwani wataalam wanakuja shambani na kutoa elimu tosha ya jinsi ya kutumia mbolea bora na kupiga dawa kwa wakati.”Monica Kilombe.

Moshi. Mpunga ni miongoni mwa zao muhimu la chakula hapa nchini na limekuwa likilimwa zaidi katika mikoa ya Mbeya, Morogoro, Shinyanga, Mwanza na baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Kilimanjro.

Kilimo hiki cha mpunga kimekuwa kimbilio la wakulima kutokana na umuhimu wake katika jamii. Licha ya kwamba zao hilo limekuwa likitegemea kilimo cha umwagiliaji, limekuwa ni mkombozi hasa kwa wakulima wanawake kwa kuwainua kiuchumi.

Katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo zao hili hulimwa zaidi katika maeneo ya chekereni, Mabogini na baadhi ya maeneo ya wilaya za Same, limechangia kwa kiasi kikubwa kuinua vipato vya wanawake ambao wamejikita katika kilimo hicho.

Ikiwa leo ni siku ya kusherehekea siku ya wanawake duniani tunamwangazia Monica Paul Kilombe (55), mkazi wa kijiji cha Chekereni, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambaye ameelezea namna ambavyo kilimo hicho kimeinua maisha yake.

Monica ambaye ni mjane analima mpunga chini ya mpango wa kidigitali kutoka Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania unaowajengea wakulima uwezo wa kulima mazao mbalimbali kisasa na kwa faida kubwa.

Mpango huo wa kidigitali wa AfricaConnect ni ubunifu wa Yara Tanzania katika juhudi za kuwakomboa wakulima wadogo na wa kati dhidi ya kadhia nyingi ambazo huwafanya wengi wao kumudu kilimo.

Meneja wa huduma ya kidigitali wa Yara Tanzania na Rwanda Deodath Mtei anasema tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022, jukwaa la AfricaConnect limewanufaisha wakulima kwa mikopo nafuu ya pembejeo, huduma za ugani na viatilifu, bima ya mazao na soko la uhakika kwa mazao yao kupitia usajili wa simu ya kiganjani.

Mtei anasema mpango huo kwa sasa unawanufaisha wakulima wa mahindi, mpunga, viazi ulaya, miwa na alizeti. Mwaka jana AfricaConnect ililenga kuwafi kia wakulima zaidi ya 300,000. “Lengo letu ni kusajili wakulima milioni moja kufi kia mwaka wa 2025,” anasema Mtei.

Hadi sasa, mikopo ya pembejeo ya Sh 2 bilioni imetolewa kwa wanufaika wa AfricaConnect. Monica ambaye ni mjane anasomesha watoto wake wanne kupitia kilimo hicho pamoja na kujenga nyumba ya kisasa ya kuishi. Mama huyo amejikwamua kiuchumi pamoja na kuweza kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

Monica anasema huduma ya AfricaConnect kutoka Yara imemletea mageuzi makubwa katika kilimo chake bila kuhangaika kama hapo zamani.

“Uzuri wake ni kwamba ukishajisajili, unapata huduma zote muhimu unazohitaji kuendeleza kilimo chako. Mpango huu umenirahisishia kuwafi kia wawezeshaji wote katika mnyororo mzima wa kilimo cha mpunga kuanzia shambani hadi sokoni,” anasema Monica.

Mwanzoni wa mwaka 2024, Monica alipata fursa ya kuwakilisha sauti ya wakulima katika kikao maalum cha mtandao cha Shirika la Biashara Duniani (WTO) kutetea hoja ya nchi wanachama kutoa nafuu ya kikodi na kisera kwa huduma za kidigitali na biashara kupitia huduma za intaneti ili kuwafi kishia wakulima wengi kama yeye mahitaji yao ya kilimo kwa unafuu zaidi.

Monica anasema kwa miaka 10 alilima bila mafanikio kutokana na elimu finyu ya kilimo bora. Anasema baada ya wakulima wa mpunga wa eneo hilo kuingia kwenye programu ya Yara, wanalima kwa tija kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo wanazopewa na kampuni hiyo. Anasema kabla ya kuingia katika programu hiyo, walikosa pembejeo na mikopo.

“Baada ya kuingia kwenye mpango wa ‘AfricaConnect’ tulikopeshwa wakulima wadogo, na kupewa mbolea na mabwana shamba wanatutembelea kila mara.”Anasema kwa misimu mitatu sasa analima kwa tija kwa kupata elimu tosha ya jinsi ya kutumia mbolea na kupiga dawa kwa wakati.”

“Tangu nipate mkopo huu nimeongeza kipato na kujenga nyumna na pia kupeleka wanangu shuleni,” anadokeza Monica. Alivyonufaika na AfricaConnect Anasema kabla ya kujiunga na mpango wa AfricaConnect alikuwa akilima kimazoea, hali ambayo ilidhoofi sha mazao yake. “Nilikuwa sijui kutumia mbegu na mbolea bora.”

Anawaasa wakulima wenzake kujiunga na Africaconnect kwani amejionea kilimo kinalipa. “Baada ya mume wangu kufariki, niliona maisha yangu ndio yameishia hapo lakini nilipambana mpaka hapo tulipokuja kupata wadau wa Yara Tanzania ambao wametusaidia kwa elimu na kutukopesha pembejeo za kilimo na kutuletea karibu watoa huduma wengine katika kilimo.”

Monica anasema alikuwa akivuna magunia 12 hadi 15 ya mpunga kwa ekari moja. Lakini baada ya kuingia katika programu ya Yara alipata lishe bora ya mimea iliyomsaidia kupata mavuno mengi zaidi.

“Baada ya kujiunga na AfricaConnect sasa ninapata wastani wa gunia 18 hadi 22 kwenye ekari moja. Nawashauri wakulima wenzangu ambao hawajajiunga na mpango huu wa kidigitali wasichekewe maana ni mzuri na hasa unatusaidia sisi wakulima wadogo.”

“Sasa hivi nimeweza kujenga nyumba yangu ya kisasa kupitia kilimo hiki na pia nimeweza kuisaidia familia yangu.” “Ndani ya miaka miwili nimeweza kuongeza shamba kutoka ekari moja niliyokuwa nayo mpaka kufi kia ekari 3 ambapo nina uwezo wa kutoa magunia 54.”

Anasema kutokana na kwamba analima kilimo chenye tija, kwa sasa ana uwezo wa kupata kilo 105 hadi 110 za mchele kwenye gunia moja la mpunga.

 Matamanio yake Anasema kwa sasa anatamani kuwa mkulima anayelimiki mashamba makubwa kwa kuwa tayari elimu anayo ya kutosha na uwezeshaji wa kutoka kampuni ya Yara Tanzania. “Tunaomba kampuni ya Yara iendelee kutuwezesha sisi wakulima wadogo ili tuweze kupiga hatua kubwa za kimaisha na natamani kufi ka mbali zaidi ya hapa.”