Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame (kulia) pamoja na Meneja Mkazi wa M & P Exploration Production Tanzania Limited, Nicolas Engel wakisaini mkataba wa mauziano ya hisa katika kitalu cha uzalishaji wa gesi asilia cha Mnazibay katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo Februari 3, 2024. Utiwaji saini huo ulishuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na taasisi mbalimbali. Picha na Ikulu