Darassa ashiriki ngoma ya Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Saa chache kabla ya kuanza rasmi mtifuano wa mechi 64 za Kombe la Dunia nchini Qatar, msanii wa Hiphop, Darassa ameshirikiana na wasanii wengine watatu kuachia ‘goma’ jipya kwa ajili ya kupandisha mizuka ya mashabiki wa soka duniani.

Dar es Salaam. Saa chache kabla ya kuanza rasmi mtifuano wa mashindano ya mechi 64 katika Kombe la Dunia la FIFA  nchini Qatar 2022, msanii wa Hipop, Darassa amekuwa mmoja wa wasanii watakaoimba nyimbo kutoa burudani kwa mashabiki wa soka.


Darassa ameshirikishwa kwenye wimbo  ‘Champion’ akiwa na  Aimaq, Sam Chilala na Jaivah.


Video ya wimbo huo  yeye mashairi ya lugha za kiarabu imeanza kusambaa katika katika mitandao ya kijamii,  tangu jana ikionyesha mandhari ya mazingira na baadhi ya viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo. 

 
“Lengo kuu sio tu ngoma hii ifike wapi ila sisi kama Taifa la Tanzania kutambulika kimataifa kwa kuwa miongoni mwa nchi zilizoandaa wimbo kwa ajili ya kombe la dunia,”amesema mzalishaji wake Abbah Process.  


Abbah anayefanya vizuri katika soko la Bongofleva amesema; “Uzalishaji ulifanyika chini ya Abbah Music nikishirikiana na Kapipo, tulianza kuiandaa hii ngoma  tangu  Julai 2021 hadi Novemba mwaka huu.”


“Wimbo (Audio) kwa ujumla imegharimu Dola za Marekani 25,000 ikiwa gharama za usafiri wa msanii kutoka Dubai kuja nchini na kurudi,”alisema.