Edo: Kuna mambo mawili uzembe na umaskini, sisi tumechagua vyote

What you need to know:

Na baada ya dogo kupewa Sh milioni moja, tujiulize. Tupo tayari kukabiliana na majanga ya usoni? Kwamba boti linaloenda Zanzibar ghafla limepata moto pale katikati watu watafikiwa kwa muda gani na waokoaji watakuwa na vifaa vipi?

Kwamba sasa hivi kuna jua kali na ukame sawa, lakini tunajiandaa vipi kukabiliana na mafuriko pindi mvua nyingi zikija?

Kwamba soko kuu la Mtwara likiungua tutawafikia watu na mali zao ndani ya dakika ngapi? Kwamba ndege ikipata ajali Ziwa Tanganyika Kigoma kutakuwa na tofauti gani na hii ya jana? Kwamba watu wakifunikwa na kifusi Chunya tutawafikia ndani ya dakika ngapi?

Kuna mambo mawili. Uzembe na umaskini. Lakini sisi tumechagua vyote. Bajeti zina mabilioni ya magari ya anasa lakini sio vifaa vya uokoaji, au sio? Tunatembea na roho mkononi.

Kwenye kuchagua namna ya kuishi tulichagua hicho hapo pichani ambacho jamaa anachagua

Imeandikwa na Edo Kumwembe