Wananchi wahofia kituo cha afya kinachofanya upasuaji kukosa jenereta

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi, George Kavinuke akiwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dk Selestini Vuru pamoja na wajumbe wa CCM na watumishi baada ya kutembea kituo .Picha na Mary Sanyiwa.

Mufindi. Kituo cha Afya Ifwagi, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa jenereta la dharula pindi umeme unapokatika unapokatika jambo ambalo ni hatari kwa shughuli za upasuaji.

Hoja hiyo imeibuka baada ya Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mufindi, George Kavinuke kufanya ziara katika Kata ya Ifwagi na kuzungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Kata hiyo.

Akizungumzia hoja hiyo, Mwenyekiti wa kituo hicho, Gerald Mwenda alisema kuwa wananchi kutoka Katika maeneo mbalimbali wamejitokeza kwa ajili ya kufuata huduma za upasuaji inatolewa kwenye kituo hicho.

Aidha Mwenda ameeleza kuwa changamoto iliyopo kwa sasa umeme kukatika mara kwa mara hasa katika kipindi hiki cha mvua hivyo wangepata jenereta la dharula ili shughuli zingine ziweze kuendelea.

Amesema kuwa endapo umeme huo ulikatika wakati shughuli za upasuaji zikiendelea jambo ambalo litakuwa ni hatari ya kupoteza maisha  ya watu kutokana na kukosekana kwa nishati hiyo ya mbadala.

"Tungepata genereta la Dharula la hata gharama ndogo kwa ajili ya kuwasaidia kupata mwanga ili shughuli za upasuaji ziweze kuendelea hata kama umeme wa Tanesco unapokatika," amesema Mwenda.

Naye mmoja wa Mkazi wa Ifwagi, Witness Mbangala amesema kuwa Serikali ifanye jitihada za makusudi ili kupeleka jenereta la dharula katika kituo hicho kwa lengo la kunusuru maisha ya wakazi hao wanaopata huduma kwenye kituo hicho.

" Tunaomba Serikali ituletee jenereta la dharula kwa kituo chethkwa sasa kimeanza kutoa huduma za upasuaji ukizingatia suala ya upasuaji ni muda wowote unaweza kutokea hivyo umeme mbadala ni muhimu sana katika kituo hicho," amesema  Mbangala.

Akijibu hoja hizo, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Selestini Vulua amesema kituo hicho ni miongoni mwa vituo sita vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambapo kinahudumia kata saba (7) na vijiji zaidi ya 30 kwa ajili ya huduma ya upasuaji.

Amesema kuwa kituo hicho kimeanza kutoa huduma hiyo 19 March 2022 hadi sasa ambapo jumla ya akina mama 148 wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji bila kupata matatizo yoyote lakini changamoto yao kubwa ni ukosefu wa generator la dharula wakati umeme unapokatika.

"Hii ni changamoto kwetu pale umeme unapokatika lakini hatuna nishati ya mbadala ya umeme pindi umeme wa Tanesco unapokatika  hali hiyo unaleta athari kubwa kwao upande wa shughuli za upasuaji," Dk Vulua.

"Unafungua tumbo la mama alafu umeme wa Tanesco unakatoka na hauna nishati mbadala ya umeme  na upo katika shughuli ya upasuaji hii ni hatari kwa mama ambaye anamfanyia  kwa sababu hii ni hatari kubwa  huwenda kinaweza kutokea kifo na kukashindwa kuendelea na upasuaji huo." Amesema  Dk Vulua

Dk Vulua ameomba Serikali na  wadau kuwasaidia kupata nishati mbadala kwa ajili ya kuteketeza majukumu yao bila kuleta madhara na shughuli za upasuaji ziweze kuendelea kama kawaida.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya hapa, George Kavinuke amesema wao kama chama kazi yao ni kuisimamia  Serikali na viongozi  hivyo watakikisha huduma hiyo inapatikana ili wananchi wa kata hiyo na vijiji jirani waweze kupata huduma zinazostahili.