Wanne wauawa kwa risasi Afrika Kusini

Maafisa wa polisi nchini Afrika Kusini wakifanya doria katika kitongoji cha KwaMashu ambapo mauaji ya watu wanne yametokea.

Muktasari:

  • Watu wanne wameuawa nchini Afrika Kusini kufuatia shambulizi la risasi kaskazini mwa Durban nchini Afrika Kusini.

Dar es Salaam. Watu watatu wameuawa papohapo kwa kupigwa risasi na mwingine mmoja kufariki akiwa hospitalini baada ya risasi kufyatuliwa katika kitongoji cha KwaMashu, kaskazini mwa Durban nchini Afrika Kusini, polisi wamesema.

Watu wengine watano waliokuwa wamejeruhiwa wamekimbizwa hospitali amesema Robert Netshiunda, msemaji wa polisi katika jimbo la pwani la KwaZulu-Natal.

"Inaripotiwa kuwa washukiwa wasiopungua 20 waliokuwa na silaha walivamia hosteli hiyo na kuwafyatulia risasi waathiriwa," amesema katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa Reuters, Polisi wamesema wanachunguza kesi za mauaji nchini humo.

Afrika Kusini ina viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani, ambapo karibu watu 20,000 huuawa kila mwaka kati ya watu milioni 60.

Siku ya Jumapili, watu wenye silaha waliwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine watatu katika ufyatulianaji wa risasi, polisi wameripoti