Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Phina ana rekodi za pekee BSS, TMA

Muktasari:

  • Huyu ni mshindi wa Bongo Star Search (BSS) 2018, mshindi wa tuzo nne za muziki Tanzania (TMA) na ana mkataba wa miaka minne wa kusambaziwa muziki wake na Ziiki Media yenye ushirikiano na Warner Music Group. Huyu ndiye Phina

Dar es Salaam. Amebarikiwa sauti nzuri inayokonga nyoyo za wengi ila uchezaji wake ni zaidi ya kuvutio kingine ndani ya Bongofleva, ingawa Phina bado hajatoa EP wala albamu, kazi aliyofanya kwa takribani miaka mitatu inatosha kumtambulisha yeye ni nani.

Huyu ni mshindi wa Bongo Star Search (BSS) 2018, mshindi wa tuzo nne za muziki Tanzania (TMA) na ana mkataba wa miaka minne wa kusambaziwa muziki wake na Ziiki Media yenye ushirikiano na Warner Music Group. Huyu ndiye Phina

1. Phina ni miongoni mwa wasanii Bongo waliofanya marekebisho kidogo katika majina yao, mwanzo kimuziki alitambulika kama "Saraphina" akalibadilisha ikawa "Phina", wengine ni Nikki wa Pili (awali, Nikki Makini), Shaa (Sarah), Nikki Mbishi (Nikki Jay).

2. Ilimchukua miaka miwili Phina kuingia rasmi katika Bongofleva baada ya kushinda BSS 2018, mwaka 2021 ndipo aliachia wimbo wake wa kwanza, In Love, kisha zikafuata nyingine kama Sitaki Tena, Sio Kitoto na Pekecha, zote zilitoka ndani ya mwaka huo.

3. Shindalo la BSS ambalo limemtoa Phina lilianza mwaka 2006, kubwa zaidi AY ndiye alikuwa msanii wa kwanza kufanya tangazo la BSS, Madam Rita Paulsen alipata fedha ya kulianzisha baada ya kampuni yake, Benchmark 360 kufanya kazi ya Wizara ya Afya.

4. Baada ya miaka 10, Phina akawa msanii mwingine wa kike kushinda TMA kama Msanii Bora Chipukizi baada ya Linah kufanya hivyo mwaka 2011, kisha Phina 2021, hapo katikati wasanii wa kiume walitawala kabla ya kipengele hicho kuanza kutoa washindi wawili.
  
Mtiririko wa wasanii chipukizi katika TMA tangu mwaka 2010 upo hivi Diamond Platnumz (2010), Linah (2011), Ommy Dimpoz (2012), Ally Nipishe (2013), Young Killer (2014), Barakah The Prince (2015), Rapcha & Phina (2021), Kontawa & Gachi (2022) na Chino Kidd (2023). 

5. Na Phina ndiye msanii wa kwanza wa Bongofleva kushinda TMA katika kipengele cha Mtumbuizaji Bora wa Kike kwa misimu miwili mfulululizo, alifanya hivyo katika tuzo za mwaka 2021 na 2022.

6. Upo Nyonyo (2022) ndio wimbo wa kwanza wa Phina kwa video yake kufikisha 'views' milioni 1 YouTube na ndio wa kwanza kufikisha 'views' milioni 10 katika mtandao huo ulioanzishwa Februari 14, 2005, huko San Mateo, California nchini Marekani.

7. Hadi sasa Phina ndiye msanii pekee wa BSS aliyeshinda tuzo nyingi za TMA ambazo nne na kuivunja rekodi ya Kala Jeremiah aliyekuwa na tuzo tatu za TMA alizoshinda mwaka 2013 kwa mpigo baada ya kufanya vizuri na wimbo wake, Dear God.

8. Otile Brown kutokea nchini Kenya ndiye msanii wa kwanza kimataifa kwa Phina kufanya naye kolabo ambapo alimshirikisha katika wimbo wake, Super Woman ulioshinda TMA 2022 kama Wimbo Bora Afrika Mashariki.

9. Phina ndiye msanii pekee wa kike Bongo aliyeshirikishwa zaidi mwaka 2022, alifanya kolabo nane ambazo ni; Natamani (Christian Bella), Yule (Stamina), Tamu (Kusah), Hata Sielewi (Barnaba),  Sinsima (Chege), Tusiachene (Dully Sykes) na Singo (Baddst 47).

10. Tangu kurejea kwa tuzo za TMA mwaka 2021, Phina ni msanii wa pili wa kike kushinda tuzo nyingi zaidi ambazo ni nne sawa na Nandy wakiwa ametanguliwa na Zuchu ambaye ameshinda saba ndani ya misimu miwili pekee aliyowania.

Mpangilio wa tuzo zote nne za TMA alizoshinda Phina upo hivi; Msanii Bora wa Kike Chipukizi (2021), Mtumbuizaji Bora wa Kike (2021), Wimbo Bora Afrika Mashariki (Super Woman) (2022) na Mtumbuizaji Bora wa Kike (2022).