Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Undercard’ ya PacMan imeshiba

MAN Pict

Muktasari:

  • Sikia hii. Bondia huyo mkongwe anarudi ulingoni, lakini kukiwa na msururu wa wakali kibao wanaomsindikiza katika pambano lake la kurejea dhidi ya Mario Barrios, Julai, mwaka huu.

NEW YORK, MAREKANI: JE unajua kwamba bondia mkali wa ngumi za uzito wa juu duniani kuanzia mwaka 1995-2021 anarudi? Unamjua Manny Pacquiao?

Sikia hii. Bondia huyo mkongwe anarudi ulingoni, lakini kukiwa na msururu wa wakali kibao wanaomsindikiza katika pambano lake la kurejea dhidi ya Mario Barrios, Julai, mwaka huu.

Jambo la kufurahisha ni kwamba ‘undercard’ ya mapambano ya kurudi ya PacMan ni tamu na ndani yake kuna ‘Mini Mike Tyson’. ‘Undercard’ ni neno linalotumika kwenye mchezo wa ngumi na pia mieleka ya kulipwa (professional wrestling) kumaanisha orodha ya mapambano ya awali kabla ya pambano kuu (main event).


Pacquiao anatarajiwa kutoka rasmi kwenye kustaafu na kupambana na Barrios kwa ajili ya ubingwa wa dunia wa WBC uzani wa welterweight, Julai 19, huko Las Vegas. Bingwa huyo wa kihistoria kuanzia flyweight hadi super welterweight tayari ameshafanya kila kitu ndani ya mchezo wa ngumi.

Hata hivyo, akiwa na miaka 46 anajiandaa kurejea kwenye ngumi za kulipwa baada ya mapumziko marefu. Mara ya mwisho Pacquiao kupigana ilikuwa Agosti 2021 aliponyang’anywa taji la WBA welterweight na Yordenis Ugas kwa uamuzi wa majaji.

Tangu wakati huo amekuwa akionekana kushuka uwezo ndani ya maonyesho ya ngumi yasiyo rasmi ambapo mapambano yake ya mwisho dhidi ya ‘kikiboksa’ wa Kijapani, Rukiya Anpo, Julai iliyopita yaliwafanya wengi waamini kwamba Pacquiao hastahili tena kupanda ulingoni. Ingawa pambano hilo la raundi tatu lilitangazwa sare, ukweli ni kwamba kama lingekuwa na alama PacMan angepoteza kwa mbali.

Pamoja na dalili za kuporomoka kwa uwezo wa mwili, WBC imeidhinisha pambano la Pacquiao dhidi ya mpinzani aliye mdogo kwake kwa miaka 17 kwa ajili ya taji la dunia la uzani wa kilo 67. Barrios alitwaa mkanda wa muda wa WBC Septemba 2023 baada ya kumshinda Yordenis Ugas na kisha kupandishwa kuwa bingwa kamili Juni alipomrithi Terence Crawford aliyepanda daraja kwenda super welterweight.

Baadaye, Barrios aliutetea mkanda wake kwa sare dhidi ya Abel Ramos kwenye ‘undercard’ ya pambano la Jake Paul dhidi ya Mike Tyson, Novemba, mwaka jana.

Ingawa pambano la Pacquiao dhidi ya Barrios halijapokewa vyema na mashabiki wa ngumi, undercard ya usiku huo inaonekana kuwavutia wengi. Kwa mujibu wa Ring Magazine, waandaaji wanapanga kuwapo pambano la marudiano kati ya Sebastian Fundora na Tim Tszyu, ambapo Fundora alimshangaza Tszyu Machi 2024 katika pambano lililowaacha wote wakiwa wametapakaa damu baada ya Tszyu kupata jeraha makubwa usoni.

Kwa ushindi huo, Fundora alitwaa mikanda ya WBO na WBC super welterweight. Hata hivyo, hivi karibuni alilazimika kuachia mkanda wa WBO baada ya kujiondoa kwenye pambano la lazima dhidi ya Xander Zayas. Ring Magazine pia imeripoti kuwa Isaac ‘Pitbull’ Cruz anatarajiwa kurejea siku hiyohiyo, huku pambano la marudiano dhidi ya Angel Fierro likitajwa kuwa miongoni mwa uchaguzi mzuri. Cruz alipigana na Fierro Februari katika pambano la kwanza tangu apoteze taji la WBA super lightweight dhidi ya Jose Valenzuela.

Pambano hilo lilikuwa la kusisimua na kutajwa kuwa ‘Fight of the Year’ wakiweka rekodi ya kurusha jumla ya masumbwi 1,410 kati yao. Cruz huwa hasumbui katika pambano la taratibu na amepata sifa kubwa kwa mtindo wake wa kushambulia kila mara, kiasi cha Mike Tyson mwenyewe kusema anamkumbusha sana alivyokuwa enzi zake.

“Ni mfupi na mwenye nguvu kwa uzani wake kama nilivyokuwa, na anamfuata mpinzani bila hofu. Tank siyo mpiganaji wa kawaida  ni wa hali ya juu. Anaweza kukushinda kwa namna mbalimbali; kwa knockout au kwa mbinu za kiufundi. Lakini Cruz, yeye ananikumbusha kabisa mimi. Anakuja na nia mbaya kabisa ulingoni,” Tyson aliwahi kuliambia Ring Magazine katika moja ya mahojiano.