Polisi kutoa maelezo kumshikilia ofisa LHRC

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesho Jumatatu Desemba 23, 2019 watatoa taarifa za Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti.

Dar es Salaam.  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesho Jumatatu Desemba 23, 2019 watatoa taarifa za Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti.

Magoti alikamatwa na polisi Ijumaa Desemba 20 eneo la Mwenge, Dar es Salaam  tukio lililozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa ametekwa.

Hata hivyo,  siku hiyo jioni polisi walieleza kuwa Magoti (26) hajatekwa na wanamshikilia pamoja na wenzake licha ya  kutoweka wazi wapo kituo gani cha polisi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Desemba 22, 2019  Mambosasa amesema, “kituo alipo ni cha polisi hatuonyeshi mtu yoyote, taarifa itatolewa kesho.”