Ndejembi mshindi Chamwino

Muktasari:
Mgombea ubunge katika jimbo la Chamwino (CCM), Deogratius Ndejembi ameshinda baada ya kupata kura 67,092 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano Oktoba 28, 2020.
Dodoma. Mgombea ubunge katika jimbo la Chamwino (CCM), Deogratius Ndejembi ameshinda baada ya kupata kura 67,092 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano Oktoba 28, 2020.
Ofisa uchaguzi wa jimbo hilo, Christina Sam amesema leo Ijumaa Oktoba 30, 2020 kuwa idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo walikuwa 98,190.
Amesema kura halali zilikuwa ni 68,082 na kura zilizokataliwa ama kuharibika zilikuwa 370.
Amesema mgombea wa chama cha CUF, Diana Simba alipata kura 990.