Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndege yaanguka hifadhi ya Serengeti Tanzania, yaua wawili

Muktasari:

Rubani na abiria wamefariki katika ajali ya ndege ndogo ya Shirika la Auric Air iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Arusha. Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.

Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete akizungumza na Mwananchi amethibitisha kutokea ajali hiyo.

"Tunatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili," amesema.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi