Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikataba tisa ya Serikali, Barrick hii hapa

Muktasari:

Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold zimesaini mikataba tisa  ya madini leo Ijumaa Januari 24, 2020.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold zimesaini mikataba tisa  ya madini leo Ijumaa Januari 24, 2020.

Makubaliano hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kushuhudiwa na Rais John Magufuli ni matunda ya mazungumzo katika ya Serikali na kampuni hiyo tangu mwaka 2017 yaliyozaa kampuni ya Twiga itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.

Mgogoro kati ya Serikali na kampuni ya Acacia iliyokuwa inasimamia migodi ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu ulianza mwaka 2017 na Rais wa Tanzania, John Magufuli akaunda tume kuchunguza mwenendo wa biashara ya madini.

Tume hiyo ilibaini ukiukwaji wa sheria, utaratibu na kanuni zilizopo hivyo kuikosesha Serikali mapato inayostahili.

Kutokana na hilo, Serikali iliipiga faini ya Dola 190 bilioni jambo lililosababisha kuanza kwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili.

Kwenye mazungumzo hayo, Acacia ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick iliwekwa pembeni na majadiliano yakafanywa na Barrick, mwisho wa siku, Acacia imefutwa sokoni na badala yake, Twiga ikachukua nafasi yake.

Katika utiliaji saini huo Tanzania iliongozwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

Wengine waliosaini mikataba hiyo ni Gabriel Malata ambaye ni naibu wakili mkuu wa Serikali, msajiliwa Hazina, Athuman Mbutuka  na Torence Ngole, kamishna msaidizi wa madini.

Mikataba iliyosainiwa

Mikataba iliyosainiwa ni mkataba wa msingi wa makubaliano, menejimenti na utoaji huduma, mkataba wa wanahisa wa kampuni ya Twiga, mkataba wa wanahisa wa North Mara.

Mingine ni mkataba wa wanahisa wa Bulyankuru, mkataba wa wanahisa wa Buzwagi, mkataba wa maendeleo ya mgodi wa North Mara, mkataba wa maendeleo ya mgodi wa Bulyanhulu na mkataba wa maendeleo wa mgodi wa Pangea.

Aidha katika hafla hiyo, Mbutuka iliwasilisha barua ya maombi ya hisa kwa Barrick na Rais wa Barrick Mark Bristow ametoa hati ya mwanahisa kwa Serikali na kumkabidhi Magufuli.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi amesema katika makubaliano hayo Serikali imepewa hisa asilimia 16 ambazo hazibadiliki hata kama Barrick itaongeza mtaji.