VIDEO: Mbowe awasili kwenye mkutano

Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akitete jambo na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchovu Mara baada ya kiwasili katika viwanja vya Nkorumo kata ya masama kati,wilayani Hai. Picha na Janeth Joseph
Muktasari:
Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe amewasili katika viwanja vya Nkoromu kata ya Masama Kati kwenye mkutano wa hadhara na kupokelewa na mamia ya wananchi.
Hai. Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe amewasili katika viwanja vya Nkoromu kata ya Masama Kati kwenye mkutano wa hadhara na kupokelewa na mamia ya wananchi.
Leo Ijumaa Februari 28, 2020 Mbowe ameanza ziara ya ya siku tano katika jimbo hilo kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Hai, John Munis amesema polisi wamewapa kibali cha kufanya mikutano hiyo.
“Mbowe atazungumza na wananchi wake pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili. Mikutano hiyo itafanya kwa siku tano mfululizo, kuanzia leo Ijumaa hadi Jumanne ijayo katika sehemu mbalimbali za Wilaya ya Hai,” amesema Munis.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema polisi wana taarifa ya mkutano huo.
'”Kiutaratibu mbunge anapokuwa na mikutano yake anapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi wilaya na taarifa za mkutano wa Mbowe tunazo,” amesema Kamanda Hamduni.