Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Irene Uwoya awaomba radhi waandishi wa habari, asema alitaka kuwatunza

Muktasari:

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya amewaomba radhi waandishi wa habari kutokana na kitendo chake cha kuwarushia fedha katika mkutano

Dar es Salaam. Msanii wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya amewaomba radhi waandishi wa habari kutokana na kitendo chake cha kuwarushia fedha katika mkutano.

Uwoya ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 17, 2019 baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na  Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ambacho pia kilimhusisha msanii mwenzake, Steve Nyerere.

Wawili hao waliitwa na Basata jana baada ya Uwoya kutumia mkutano wa wasanii  na waandishi wa habari kuwarushia fedha jambo lililozua mjadala ikiwamo kuonyesha dharau kwa wana taaluma hao.

“Mimi binafsi naomba samahani lakini sikufanya makusudi kama watu walivyotafsiri, nilifanya hivyo kwa furaha zangu tu kwa kuwa mlikuja kwa wingi,” amesema Uwoya.

Amebainisha kuwa hakukuwa na mpango wa kuwadhalilisha waandishi wa habari, na kwamba alilenga kuwatunza lakini ametafsiriwa vibaya.

Leo wawili hao walifika Basata kuitikia wito wa baraza hilo. Walifika saa 4:30 na gari aina ya Toyota Prado nyeusi.

Kabla ya kushuka walikaa zaidi ya robo saa ndani ya gari huku waandishi waliofika hapo wakiwa wametegesha kamera zao kusubiri kuwachukua picha.

Ilipofika saa 4:45 asubuhi wasanii hao walishuka kwenye gari hilo na kuelekea ndani ya ofisi ya Katibu Mtendaji wa Basata.