Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ilichokisema TIC kuhusu korosho

Muktasari:

  • Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  kimesema kitashirikiana na kituo cha utafiti wa zao la korosho cha Naliendele kuhakikisha wakulima wengi wa zao hilo wanapata elimu ya namna ya kuzalisha bidhaa nyingi zitokanazo na korosho

Dar es Salaam. Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  kimesema kitashirikiana na kituo cha utafiti wa zao la korosho cha Naliendele kuhakikisha wakulima wengi wa zao hilo wanapata elimu ya namna ya kuzalisha bidhaa nyingi zitokanazo na korosho.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Julai 24, 2019 na mkurugenzi wa TIC,  Godfrey Mwambe wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu kongamano la korosho mkoani Mtwara lililofanyika wiki iliyopita.

Mwambe amesema wakati wa kongamano hilo lililowashirikisha watu 400 wakiwemo 150 kutoka nchi mbalimbali duniani, walitembelea kituo cha utafiti cha Naliendele na kubaini zaidi ya bidhaa nane zinazotokana na zao la korosho.

"Kilichowafurahisha watu ni kituo cha utafiti cha Naliendele, kwa kiasi kikubwa zao la korosho limeonekana kuzalisha bidhaa nyingi zikiwemo maziwa, juice, mvinyo, spirit, unga kwa ajili ya kutengeneza chokolate na biskuti,  poda na hata vilainishi kwa ajili ya mashine mbalimbali,” amesema.