Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Billnass aeleza jinsi mpenzi wake ‘alivyowalinda’ na Nandy

Muktasari:

Msanii Billnass amesema mpenzi wake (hakutaka kumtaja jina) alimfuata 'location' na wakiwa na Nandy wanapiga picha za wimbo wa ‘Bugana’ na kulazimika kuwa mlinzi kwa muda ili kuhakikisha hawafanyi kitu tofauti na walichokifuata.


Dar es Salaam. Billnass ambaye ni msanii wa muziki wa bongofleva nchini Tanzania amefunguka jambo ambalo mpenzi wake wa sasa alimfanyia wakati alipokuwa akirekodi wimbo wa ‘Bugana’ alioimba na Nandy.

Billnass amesema hayo alipozungumza na kipindi cha MCL Extra ambacho kinarushwa  kwenye chaneli ya MCL Digital ikiwa ni siku chache tangu aachie wimbo huo.

Amesema  alimuaga anakwenda kupiga picha za wimbo huo kwa kushirikiana na Nandy, lakini mpenzi wake kwa sababu ya wivu hakumuamini na kulazimika kujiunga nao eneo la tukio.

Amesema wakiwa wanapiga picha hizo yeye pamoja na Nandy, mpenzi wake alikuwa akiwatizama mwanzo hadi mwisho walipomaliza.

“Wivu ulimfanya asiamini kama ninakwenda kweli kupiga picha tu, hivyo akaja na kunilinda mwanzo mwisho, ”amesema Billnass

Billnass ametoa ufafanuzi huo mara baada ya kuulizwa mpenzi wake anachukuliaje anapomuona yupo karibu na Nandy.

Wimbo huo wa Bugana umejizolea umaarufu kwa muda mfupi huku kikubwa ukichochewa na wawili hao kuwahi kuwa katika mahusiano.

Amesema wimbo huo alimtungia Nandy tangu mwaka 2016 kwa lengo la kubadili muziki wake, hivyo walichokifanya kwa sasa ni kuuboresha mashairi yake kidogo.

Hata hivyo, Billnass hakuwa tayari kuzungumzia kwa kina kuhusu mpenzi wake wa sasa akisema wakati ukifika atafanya hivyo.

Akijibu swali la lini hasa anakusudia kuoa, msanii huyo amesema, ‘ndani ya miaka kumi’ hivi ninatarajia kufanya hivyo.