Magufuli amtaka Majaliwa achape kazi adumu madarakani

Rais wa Tanzania, John Magufuli
Muktasari:
Amemwambia hayo leo alipomwapisha Ikulu ya Chamwino
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania John Magufuli amesema nafasi aliyompa Waziri mkuu haina uhakika bali itategemeana na utendaji wake.
Ameyasema hayo leo katika hafla ya kumwapisha Waziri mkuu, Kassim Majaliwa sambamba na Waziri wa fedha na Mpango, Philip Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi iliyofanyika Ikulu Chamwino jijiji Dodoma
Amesema amekuwa akisikia baadhi ya watu na vyombo vya habari vikisema Waziri mkuu Kassim Majaliwa amechaguliwa kuongoza kwa miaka mitano mingine, huku akibainisha kuwa utendaji kazi wake ndiyo utakao mweka katika nafasi hiyo.
“Kwa hiyo tumuombee ili angalau afikie rekodi ya Sumaye (Waziri Mkuu mstaafu) miaka mitano aliyo na guarantee (uhakika) nayo ni aliyomaliza. Hii mingine ni propability (haina uhakika), amesema na kuongeza:
“Na mawaziri niliowateua na nitakaowateua hawana ‘guarantee’ (uhakika) kwa sababu sisi tumezunguka kuahidi kuwa wananchi kupitia Ilani ya chama na wametuamini kwa kura nyingi, imani yao lazima iendane na tutakayofanya, tuilipe, tuitimize kwa nguvu zote,”amesema.