Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mr kuku aiangukia Serikali kuhusu mali zake

Muktasari:

Ataka zisiuzwe na mahakama

Dar es Salaam. Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29), maarufu kama Mr Kuku, anayekabiliwa  na kesi ya kufanya biashara haramu ya upatu  kwa kukusanya fedha za umma zaidi ya Sh 17bilioni, ameiomba Serikali imsaidie ili mali zake zisiuzwe na Mahakama.

Ameomba hilo baada ya watu waliowekeza fedha zao katika biashara ya kuku kumfungulia kesi ya madai, katika Mahakama ya Mwanzo KIgamboni wakidai fedha zao .

Machibya anakabiliwa na mashtaka saba likiwamo la kusimamia biashara ya upatu, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 60/2020 iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Machibya amesema hayo leo, Novemba 16,2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo  Janeth Mtega wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

" Mheshimiwa hakimu nimefunguliwa kesi ya madai mahakama ya mwanzo Kigamboni na watu ambao waliwekeza fedha zao katika mradi wa kuku na taarifa nilizopewa ni kwamba hukumu imeshatolewa na mahakama hiyo na  baadhi ya mali zangu zinatakiwa kuuzwa" amesema Machibya na kuongeza.

" Kutokana na hali hii, naomba upande wa mashtaka wanisaidie juu ya jambo hili kwa sababu huku kesi niliyofunguliwa bado haijaisha.’’

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alimtaka mshtakiwa huyo awapatie nyaraka za kesi hiyo ili waweze kuziwasilisha Idara ya upelelezi kwa ajili ya hatua nyingine.

Hakimu Mtega baada ya kusikiliza hoja za upande zote, alisema hawezi kutoa uamuzi juu ya hoja zilizotolewa na mshtakiwa kwa sababu kesi hiyi iko mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, ambaye atatoa uamuzi tarehe ijayo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mtega aliahirisha kesi hadi Novemba 30, itakapotajwa.

Kesi hiyo imendeshwa kwa njia ya video na mshtakiwa yupo rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili kutokuwa na  dhamana kwa mujibu wa sheria.