Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamacu chapatiwa mbinu ya kuongeza thamani ya korosho

Muktasari:

Kinatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda cha usindikaji wa vyakula

Mtwara. Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi na Mtwara(Mamacu) mkoani Mtwara kimetakiwa kuongeza maghara ya kuhifadhia zao la korosho sanjari na kuanza ujenzi wa viwanda vya ubanguaji wa korosho ili kuongeza thamani ya zao la korosho hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Khatibu Kazungu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego wakati wa Mkutano Mkuu wa 17 wa chama hicho uliofanyika mjini hapa.

Alisema kwa sasa Serikali ina mkakati wa kuhakikisha kabla ya kufika mwaka 2019 viwanda vya ubanguaji wa korosho viwe vimeshajengwa.

Mkuu huyo wa wilaya hiyo alisema, chama kikuu hakina budi kuendelea kubuni miradi mbalimbali itakayo kiwezesha kushindana sokoni. Alisema wakati umefika kwa vyama vya ushirika kuangalia mazao mengine ya biashara badala ya kutegemea zao moja la korosho.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamacu, Kelvin Rajabu alisema wanatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda cha usindikaji wa vyakula vya aina mbalimbali katika eneo la viwanda la Mitengo, Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Rajabu alisema kiwanda hicho kitasindika bidhaa mbalimbali ikiwamo ufuta na utengenezaji wa juisi, jambo ambalo litasaidia kuwawezesha wakulima wa korosho kujiongezea kipato.

Hata hivyo, alisema ujenzi huo unatarajiwa kuanza rasmi Desemba mwaka huu na utagharimu zaidi ya Sh1 bilioni na kutoa ajira 100 kwa wakazi wa Mtwara ambazo zitawasaidia kujikwamua kimaisha.