Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabia za wanawake zinazokera wanaume lakini hawasemi

Muktasari:

Miongoni mwa tabia hizo ni kuwafanya wao kama kitega uchumi chao. Wanaume wengi hunung’unika kwa marafiki zao kuhusu wanawake wenye hizo tabia. Ukiwakuta kijiweni wanafunguka ile mbaya.

Dar es Salaam.  Waswahili husema, ‘mtaka cha uvunguni sharti ainame’ huenda ndivyo ilivyo kwa baadhi ya wanaume ambao wanashindwa kuwapa makavu ‘laivu’ wanawake wenye tabia zinazowakwaza.

Miongoni mwa tabia hizo ni kuwafanya wao kama kitega uchumi chao. Wanaume wengi hunung’unika kwa marafiki zao kuhusu wanawake wenye hizo tabia. Ukiwakuta kijiweni wanafunguka ile mbaya.

Mtandao wa masuala ya mahusiano (eHarmony advice) umetaja tabia hizo za wanawake zinazowakera wanaume.

Kupenda mambo makubwa kupita uwezo wao. Hii tabia inawakera wanaume waliowengi wakati mwingine wanashindwa kuwaambia wanawake, wanajikaza na kujitutumua ili waonekane vidume. Unakuta mwanaume ana uwezo wa kununua nyama mara mbili kwa wiki lakini mwanamke analazimisha kula nyama kila siku.

Watu wa maslahi. Wanaume pia hukerwa na tabia ya wanawake ambao wako kimaslahi. Hawa ni wanawake ambao kama amekupenda ukiwa na pesa siku mambo yakienda mrama ujue na mapenzi yameisha.

Kuwa king’ang’anizi. Kuna wanawake wanapenda kuganda kama kupe. Wakati mwingine wanaume wanahitaji muda wao binafsi kama ilivyo kwa wanawake lakini mtu akiambiwa hivyo haelewi. Tabia hii inawakera wanaume.

Kusikiliza mambo au watu wa nje zaidi. Ukipita kwenye kijiwe zaidi ya kimoja huwezi kukosa wanaume wakiwa wanazungumzia kuhusu tabia hii hasa kwa wale walio na wenza. Wanaume hukerwa na tabia ya mwanamke kuendekeza na kuyapa kipaumbele mambo ya nje ambayo mara nyingi huvuruga familia au mahusiano.