Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upelelezi kesi ya Mfanyabishara Zakaria haujakamilika

Mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa, Peter Zakaria 

Muktasari:

Kesi kutajwa tena Septemba 10


Musoma. Kesi mbili zinazomkabili mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa, Peter Zakaria zimepangwa kutajwa tena Septemba 10, 2018 baada ya upelelezi wa kesi hizo kutokamilika.

Zakaria anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni jaribio la kuua pamoja na uhujumu uchumi ambapo baada ya kukosa dhamana katika kesi ya pili mfanyabiashara huyo yupo mahabusu tangu Juni 29, 2018 alipokamatwa na polisi.
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mara, Rahimu Mushi amesema mahakamani hapo leo Agosti 27, 2018 kuwa kesi hizo kwa pamoja zitakuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa tena Septemba 10 baada ya kuombwa na upande wa mashtaka.

Awali mwanasheria wa Serikali Samuel Lukelo ameiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hizo kutajwa tena kutokana na upelelezi wa kesi  zote mbili kutokamilika.

Kufuatia ombi hilo, wakili anayemtetea Zakaria, Onyango Otieno ameomba upande wa Jamhuri kueleza mahakamani hapo hatua iliyofikiwa katika upelelezi wa kesi zote.
Kutokana na ombi hilo wakili wa serikali, Lukelo amesema upelelezi wa kesi hizo unahitaji majibu ya kitaalamu na katika shtaka la kwanza la kujaribu kuua, upelelezi bado unaendelea na kwamba bado ofisi yake haijapokea fomu namba tatu kuelezea hali za majeruhi wawili waliojeruhiwa kwa kupigwa risasi na mtuhumiwa huyo.
Lukelo amesema majeruhi hao walipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ingawa hakutaja nchi walikolazwa majeruhi hao ambao ni maofisa usalama wa taifa.
Kuhusu upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi, Lukelo amesema suala hilo limepelekwa kwa mtaalam wa milipuko kwa ajili ya uchunguzi wa silaha aliyokutwa nayo mtuhumiwa akimiliki kinyume cha sheria.
"Bado hatujapata fomu namba tatu kuelezea hali za majeruhi zinaendeleaje ila taarifa ni kwamba bado wanaendelea na matibabu nje ya nchi vile vile silaha aliyokutwa nayo imepelekwa kwa mtaalam wa milipuko kwa majibu ya kitaalam zaidi," alisema Lukelo. 
Zakaria alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mara Julai 5 mwaka huu kwa kosa la kujaribu kuua ambapo alidaiwa kuwapiga risasi maofisa usalama wa Taifa wawili mjini Tarime Juni 29 walipofika katika moja ya kituo cha mafuta kinachomilikiwa na mfanyabiashara huyo kwa lengo la kujaza mafuta kwenye gari yao.
Baada ya kufikishwa mahakamani hapo Zakaria hakupewa dhamana badala yake kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 10 baada ya kuibuka hoja za kisheria.
Julai 10 mfanyabiashara huyo alifikishwa mahakamani na kupewa dhamana hata hivyo alirudishwa mahabusu baada ya kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi baada ya kupatikana na bunduki aina ya shotgun inayodaiwa alikuwa akiimiliki kinyume cha sheria.