Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sumaye augua ghafla, alazwa hospitali Tanga

Muktasari:

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema nchini Tanzania, Frederick Sumaye amelazwa katika Hospitali ya Bombo jijini Tanga baada ya kuagua ghafla


Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameugua ghafla akiwa mkoani Tanga.

Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema amepatwa na tatizo la afya akiwa katika majukumu ya kichama.

Taarifa iliyotolewa leo mchana Ijumaa Februari 8, 2019 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa Chadema, Tumaini Makene imesema, “Sumaye alikuwa mkoani Tanga, akiendelea na ratiba ya ziara ya shughuli za chama kabla ya kupatwa na shida ya afya ghafla leo asubuhi.”

“Baada ya kutibiwa hali yake inaendelea vizuri na sasa amepumzika wakati mipango ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo hii kwa ajili ya uchunguzi zaidi ikifanyika.”

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi