Mwalimu aliyemchapa mwanafunzi hadi kufa, ahukumiwa kunyongwa

Muktasari:

  • Leo Jumatano, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemhukumu kunyongwa hadi kufa, mwalimu Respicius Mutazangira baada ya kumkuta na hatia ya kuhusika na kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius huku ikimwachia huru Heriet Gerald.

Bukoba. Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemhukumu kunyongwa hadi kufa, mwalimu Respicius Mutazangira baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius mwishoni mwa mwaka 2018.

Wakati Respicius akihukumiwa kunyongwa, mwalimu mwenzake ambaye alishtakiwa naye, Heriet Gerald ameachiwa huru.

Hukumu  hiyo imetolewa leo na Jaji Lameck Mlacha ambaye alisikiliza kesi hiyo kwa mwezi mmoja.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa walimu hao walitenda kosa la kumuadhibu kwa kipigo Sperius kwa madai kuwa aliiba mkoba wa mwalimu Eliet ukiwa na fedha.

Endelea kufuatilia zaidi kupata undani wa kinachojiri mahakamani