Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malkia wa Tembo jela miaka 15

Muktasari:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka 15 jela washtakiwa watatu akiwemo Malkia wa Tembo kwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.

 


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka 15 jela washtakiwa watatu akiwemo raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu Malkia wa Tembo.

Kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh13bilioni.

Mbali na Glan, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 21/2014  ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

Hukumu hiyo umetolewa leo mchana Februari 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi baada ya kuwatia hatiani washtakiwa hao.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi