Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lowassa atua Monduli kwa kishindo

Muktasari:

Lowassa apokelewa kwa shangwa na wafuasi wa CCM akiwamo mbunge wa jimbo la Monduli, Julius Kalanga

Monduli. Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa ametua wilayani Monduli na kupokewa kwa shangwe na wafuasi wa CCM ambao wamekusanyika viwanja vya CCM Monduli.

Lowassa alifika Monduli majira ya saa 7:34 na kushuka kwenye gari na kupokewa na mbunge wa jimbo la Monduli, Julius Kalanga.

Baada ya kushuka kwenye gari, Lowassa aliwapungia mkono wafuasi wa CCM ambao walilipuka kwa shangwe na vigelegele.

Lowassa baada ya kushuka alikwenda moja kwa moja ofisi za CCM wilayani Monduli ambapo hadi sasa kikao kinaendelea ambacho anashiriki pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole.

Baada ya kikao hicho ambacho kinajumuisha wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Monduli, Lowassa atakabidhiwa kadi ya CCM.