Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

IGP Sirro awatoa hofu wananchi tishio la ugaidi Tanzania

Muktasari:

IGP Simon Sirro amezungumzia taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania iliyotoa tahadhari ya kutokea kwa ugaidi katika hoteli za Masaki na maduka ya Slipway, Msasani Peninsula Jiji la Dar es Salaam akiwataka wananchi kutokuwa na hofu.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewatoa hofu wananchi juu ya tishio la ugaidi katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, likisema taarifa hizo zimeshaanza kufanyiwa kazi.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro ameiambia Mwananchi usiku huu Juni 18, 2019 kuwa jeshi lake lilishapata fununu za shambulio hilo kabla Ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari juu ya tukio hilo kupitia tovuti yake Juni 18, 2019.

Akizungumzia taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, IGP Sirro amesema, “hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo. Tangu jana (Jumanne Juni 17, 2019) tulipata hiyo taarifa kwa hiyo tuko vizuri, timu zetu za operesheni na intelijensia na wengine tunaifanyia kazi.”

Katika tangazo lake Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania inaeleza kuwapo kwa uvumi wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika eneo la Masaki hususan hoteli za kitalii na maduka ya maeneo hayo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Ubalozi huo umewataka wakazi kuwa makini na maeneo hayo, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.