Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fedha za wateja zawazulia balaa watumishi watatu

Muktasari:

Waliosimamishwa kazi ni mhasibu wa mamlaka hiyo, Johnson Rugemalira; msoma mita za maji, Justus Justiniani na Verdiana Nyamkara.

Igunga. Fedha zilizolipwa na wateja wa huduma ya maji kwa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira mjini Igunga (Iguwasa), mkoani Tabora, zimegeuka kaa la moto kwa watumishi watatu ambao wamesimamishwa kazi ili wachunguzwe kwa tuhuma za kuzitafuna.

Waliosimamishwa kazi ni mhasibu wa mamlaka hiyo, Johnson Rugemalira; msoma mita za maji, Justus Justiniani na Verdiana Nyamkara.

Akizungumzia watumishi hao mwishoni mwa wiki iliyopita, mkurugenzi mtendaji wa Iguwasa, Raphael Merumba alisema wamesimamishwa kazi baada ya kubaini kuwa Sh4 milioni fedha za ankara za maji walizokuwa wakikusanya kwa wateja zilikuwa hazifikishwi ofsini.

Merumba alisema kwa sasa wanasubiri kikao cha bodi ya maji ambacho kitafanyika mwezi huu kujadili jambo hilo na endapo watakutwa na hatia hatua zingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mkurugenzi huyo aliwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kuachana na tamaa za kuchukua fedha zinazolipwa na wateja wanaowahudumia.

“Kamwe hatutasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtumishi yeyote atakayebainika kuiba fedha za ankara za maji zinazolipwa na wateja,” alisisitiza.

Akizungumzia tuhuma za kutafuna fedha, Rugemalira alisema hajafanya ubadhirifu wowote wala hajawahi kuwafuata wateja kwa lengo la kuchukua fedha zao.

“Kwa ufupi haya ni majungu yanayolenga kunichafulia kazi yangu,” alisema.

Wateja zaidi ya 30 waliolipa ankara za maji na fedha zao kudaiwa kutafunwa akiwamo mfanyabiashara wa nyumba za kulala wageni aliyelipa Sh700,000, Msafiri Lugega aliyesema uaminifu ni jambo kubwa na muhimu maishani.