Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwakyembe amlilia anayedaiwa kuchora nembo ya taifa

Muktasari:

· Ngosha alikuwa akiishi maisha duni huko Buguruni Malapa

·Akitegemea kipaji chake cha uchoraji kujipatia kipato

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya msanii mkongwe katika fani ya uchoraji Mzee Francis Maige Kanyasu (86), aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Habari, imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe  amemwelekeza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Mngereza, kushirikiana kwa karibu na ndugu na jamaa wa marehemu katika mazishi yake.

 

“Wizara itahakikisha michango ya wasanii wakongwe kama Mzee Kanyasu, inafuatiliwa kwa karibu na kuwekewa kumbukumbu kwa faida ya vizazi vijavyo.” imesema taarifa hiyo