Vyakula hivi si vya kukosa kwa kila mtu

Muktasari:
Mkurugenzi wa idara ya kinga kutoka Taa-sisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Crispin Kahesa anasema kila chakula kina umuhimu na mchango wake katika kujenga na kuupa mwili nguvu.Anasema baadhi ya vyakula vinasaidia kupunguza kemikali zinazosababisha sara-tani. “Saratani ni ukuaji wa chembechembe hai zinazokuwa bila mpangilio, hata hivyo mwili wetu unaanza kujengwa na chem-bechembe hai moja na baadaye zinaun-ganika na kuwa nyingi na hatimaye kuwa chembechembe hai zinazotengeneza tishu zenye baadhi ya ogani,” anasema Dk Kahesa.
Watalaamu wa masuala ya lishe wanasema hakuna dawa au chakula cha kula siku moja cha kuponya tatizo la kushuka kwa kinga ya mwili, badala yake jamii inatakiwa kula mlo wenye mpangilio unaokubalika.Wanabainisha kuwa njia nzuri ya kuka-biliana na tatizo hilo ni kula matunda, mboga za majani, vyakula vya nafaka na maji ya kunywa ya kutosha.
Mkurugenzi wa idara ya kinga kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Crispin Kahesa anasema kila chakula kina umuhimu na mchango wake katika kujenga na kuupa mwili nguvu.Anasema baadhi ya vyakula vinasaid-ia kupunguza kemikali zinazosababisha saratani. “Saratani ni ukuaji wa chem-bechembe hai zinazokuwa bila mpangilio, hata hivyo mwili wetu unaanza kujengwa na chembechembe hai moja na baadaye zinaunganika na kuwa nyingi na hatimaye kuwa chembechembe hai zinazotengeneza tishu zenye baadhi ya ogani,” anasema Dk Kahesa.Anavitaja baadhi ya vyakula vyenye uwezo wa kupambana na saratani kuwa ni vyote vyenye vitamini na vina mchango mkubwa katika kuzuia saratani.Anasema kuna baadhi ya vyakula vina-jenga kinga ya mwili na kuna vingine vin-achochea saratani kutokea kutokana na mazingira.Wakati Dk Kahesa akisema hayo, Muu-guzi kutoka Shirika la Watawa la Mab-inti wa Maria Immakulata (DMI), Farida Mathola anavitaja baadhi ya vyakula na matunda yanayopambana na kuzuia sara-tani kuwa ni maboga, karoti, viazi vitamu, pilipili nyekundu na zile za njano.
Vingine ni bilinganya, binzari, broccoli, nyanya, majani ya ngano huku kitunguu saumu kikionyesha uwezo wa kuondoa hatari ya kupatwa na saratani ya tumbo, koo na matiti kwa mtu anayetumia mara kwa mara.Farida anasema mboga za majani zenye rangi ya kijani zina uwezo mkubwa wa kupambana na Saratani huku spinachi ikiwa inaongoza kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini au kuon-doa hatari ya kupatwa na saratani ya ini, kizazi, utumbo mpana na kibofu cha mkojo.
“Kutokana na hali hiyo, jamii inaweza kuzi-weka mboga hizi katika orodha ya vyakula vya kila siku, hasa ukizingatia umuhimu wake wa kupambana dhidi ya magonjwa ya kansa na kuwapo kwa kiwango kingi cha Vitamin E, ambayo nayo ni muhimu kwa kinga ya mwili,” anasema Farida.
Anafafanua kwa upande wa matunda, stafeli, barungi, tufaa, machungwa na nanasi ni miongoni mwa yanayotajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na saratani huku nanasi likiwa na kimeng’enyo cha aina ya ‘bromelain’, ambacho ni muhimu kwa kinga dhidi ya saratani ya matiti na mapafu na pia, lina vitamin C inayoongeza kinga mwilini.
Pia, tufaa lina kirutubisho muhimu kiitwacho ‘quercetin’ kilichoonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza hatari ya mtu kupatwa na saratani ya mapafu na ina . Pia, uwezo wa kupunguza kasi ya kukua kwa seli za kansa ya kibofu. Muuguzi huyo anaelezea kwa ufupi baadhi ya faida zilizopo kwenye vyakula na matunda yanayozuia Saratani kwa binadamu.
Kuwa moja ni pamoja na majani ya ngano, sharubati ya majani ya ngano nayo husaidia kuimarisha protini kwenye seli nyekundu za damu na kuimarisha kinga ya mwili na mfumo wa kusaga chakula na kuondoa lehemu.
Pia, majani hayo huimarisha mfumo wa sukari mwilini na kutibu wenye matatizo ya kisukari. Huimarisha na kutibu matatizo ya ini, figo na kuondoa sumu mwilini.
Barungi lina wingi wa asidi ya citric, potassium na calcium na mtu anapokula tunda hilo usiku wakati wa kwenda kulala humfanya apate usingizi mzuri.
Lakini unywaji wa juisi ya tunda hilo asubuhi kabla ya kula chakula kingine, huondoa tatizo la kukosa haja kubwa na kuongeza hamu ya kula pamoja na kusaidia uyeyushaji wa chakula mwilini, lakini pia hupunguza homa itokanayo na mafua makali.
Barungi hutibu pia magonjwa ya kiharusi, hupunguza rehemu, unene, kukarabati mishipa ya damu na kuipa damu uwezo wa kutembea mwilini.
Binzari au manjano
Licha ya watu wengi kutumia binzari kama kiungo, lakini kina faida nyingi mwilini ikiwamo ya kuzuia hatari ya kupata saratani.
Ulaji wa binzari mara kwa mara huimarisha afya ya macho, viungo vya mwili na utendaji kazi wa ini. Lakini pia huimarisha chembe hai za mwili na mfumo wa uzalishaji mbegu za uzazi.
Tikitimaji chungu
Kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa kwenye Jarida la Utafiti wa Kansa, majimaji yanayotolewa katika tikitimaji chungu yanayojulikana kama ‘karela’ kwa kihindi, hupunguza kasi ya kukua kwa seli za sarataniya matiti.
Utafiti huo ulioongozwa na mtafiti Ratna Ray, unaeleza tikitimaji chungu lina uwezo wa kuzuia saratani ya matiti, lakini bado haijathibitika kama majani yake yanauwezo wa kutibu ugonjwa huo.
Brokoli (Broccoli)
Miongoni mwa faida iliyopo katika mboga hiyo ni kuzuia mwili kupatwa na saratani. Kwa sababu ina glucoraphanin ambayo hubadilishwa mwilini na kuwa sulforaphane inayozuia saratani.
Pia, broccoli husaidia mfumo mzima wa neva na ubongo kufanya kazi inavyotakiwa, huipatia misuli nguvu, lakini pia huimarisha msukumo wa damu na hupunguza sumu mwilini kwa kusafisha uchafu
Kitunguu Saumu
Licha ya kutibu magonjwa zaidi ya 30, kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini kikielezewa kuwa na faida katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo kwenye mapafu, mfumo wa umeng’enyaji chakula na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Ulaji wa mara kwa mara wa kiungo hicho huondoa sumu mwilini, husafisha tumbo, huyeyusha mafuta mwilini, husafisha njia ya mkojo na hutibu UTI na kuondoa amoeba, minyoo na bakteri wengine.
Lakini pia kiungo hicho kina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume na hutibu matatizo ya kukosa nguvu za kiume.
Bilinganya
Ni aina ya mboga inayopatikana katika kundi la mbogamboga, lakini pia inaweza kutengenezwa juisi ambayo husaidia kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo.
Virutubisho vilivyopo katika mboga hiyo husaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi na ngozi ya bilinganya inaambatana na miseto iitwayo terpenes inayosaidia kupunguza lehemu mwilini.
Stafeli
Asilimia 12 ya tunda hilo lina sukari ya asili na ni salama kwa mlaji na ni chanzo kikuu cha vitamini C, madini ya chuma na Niacin Riboflavin huku likiwa na kirutubisho aina ya Annona Muricata chenye uwezo wa kukabiliana na maradhi ya saratani. Tunda hilo huzuia matatizo ya mfumo wa fahamu, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, hudhibiti ukuaji wa bakteria, virusi, vijidudu nyemelezi, hutibu majipu na uvimbe, huongeza stamina ya mwili na kurahisisha kupona haraka, hufukuza chawa na kuzuia magonjwa yasaratani.
Utafiti uliowahi kufanyika, unaonyesha juisi ya stafeli hutibu saratani kwa haraka kwa sababu inanguvu mara 10,000 zaidi ya tiba ya mionzi katika kuzia seli za saratani.
Nyanya:
Moja kati ya faida ya nyanya katika mwili wa binadamu ni kulinda uharibifu wa DNA kutokana na wingi wa antioxidants, vitamin C na A ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kulinda DNA isishambuliwe, lakini nyanya hiyo husaidia kukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa kisukari.
Nyanya huzuia saratani ya tumbo, mapafu, koo na saratani ya kizazi, lakini ulaji wa nyanya kwa wingi huzuia saratani ya tezi dume na hupunguza kiwango cha sukari mwenye damu, husaidia kusafisha ngozi, husaidia macho kuona vizuri hasa nyakati za usiku.
Nini kifanyike?
Luitfrid Nnally ni mtaalamu wa Masuala ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Nchini ( TFNC), anasema ili kukabiliana na tatizo la saratani, ni lazima kuwapo na maandalizi bora ya chakula kabla ya kupikwa ili virutubisho vilivyopo visiweze kupotea.
Dk Kahesa ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya Saratani anasisitiza ili jamii iweze kukabiliana na saratani na magonja menginie, inatakiwa kula vyakula hai na halisi badala ya vilivyosindikwa. “Kuna baadhi ya watu wanaondoa virutubisho bila kujua, mfano unatengeneza juisi ya embe halafu unaongeza radha, unakuwa umeweka kemikali na unaua baadhi ya virutubisho hai vilivvyokuwapo kwenye tunda lako,” anasema Dk Kahesa.