Simba kuhamia gym

KOCHA Msaidizi wa Simba, Denis Kitambi ameamua kuhamishia mazoezi yake kwa siku tatu gym  baada ya kufanya mazoezi ya uwanjani kwa siku tatu.
Kitambi alikuwa akifanya mazoezi mbalimbali kwa maana ya nguvu, mbinu na mengineyo ambayo yote walikuwa wakifanya uwanjani.
Kitambi alisema kesho Jumamosi hawatafanya tena mazoezi ya uwanjani bali watakwenda kufanya mazoezi ya Gym.
"Tutafanya mazoezi ya Gym  zilizopo Golden Tulip Tower ili kuweka miili sawa ya wachezaji kwani walitumika zaidi uwanjani,"
"Ambalo lipo mbele yangu kwa wakati huu ni kuandaa timu kuwa fiti na hali ya ushindani lakini kuhusu kucheza mechi za kirafiki hili bado sijaambiwa na uongozi," alisema.
Kitambi alisema kuhusu taarifa za kuondoka kwa Patrick Aussems na kuja kocha mwingine kuchukua nafasi yake hilo halifahamu.
"Ninachofahamu ni kwamba kocha wa Simba ni Aussems, sifahamu lingine kuhusu yanayoendelea juu ya kocha," alisema Kitambi.