Makipa wa Barcelona, Bayern warushiana maneno kuhusu kuwekana benchi timu ya taifa

Muktasari:

  • Pamoja na kutajwa na Fifa kuwa mmoja wa makipa bora watatu duniani, mlinda mlango wa Barcelona, Marc-Andre Ter Stegen amekuwa akiwekwa benchi timu ya taifa ya Ujerumani.

Kipa wa Barcelona, Marc-Andre Ter Stegen jana Jumatatu alimtuhumu Manuel Neuer kuwa anatoa maoni "yasiyo sahihi" katika vita ya maneno baina ya makipa hao wawili wa timu ya taifa ya soka ya Ujerumani.

Mzozo kati ya makipa hao uliibuka baada ya Ter Stegen kueleza alivyofadhaika baada ya kutopangwa katika mechi ya timu ya taifa mwishoni mwa wiki iliyopita.

"Sidhani kama ni jukumu la Manuel kutoa maoni yake kuhusu hisia zangu," alisema Ter Stegen jana kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baina ya Barcelona na Borussia Dortmund.

Ter Stegen, kipa ambaye hana mpinzani katika kikosi cha kwanza cha Barcelona, amekuwa akipata shida kumpiku Neuer katika kikosi cha kwanza cha Ujerumani, na alidai ilikuwa "ni pigo gumu" kukaa benchi wakati wa mechi za michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali zijazo za Mataifa ya Ulaya, Euro 2020 mapema mwezi huu.

Neuer alijibu vikali maoni ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 27, akisema kuwa Ter Stegen aliiumiza timu kwa kutoa maoni hayo hadharani.

Jumatatu, Ter Stegen alijibu mapigo, akizungumzia maoni ya Neuer kuwa "hayakuwa sahihi".

"Kila mmoja ameona jinsi nilivyokuwa katika miaka michache iliyopita," alisema.

Kipa huyo wa Barcelona amekuwa akitajwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fiufa) kama mmoja wa makipa bora watatu duniani katika miezi 12 iliyopita.

Ter Stegen alionyesha kiwango kizuri wakati aliposhika kwa muda nafasi ya Neuer kati ya mwaka 2017 na 2018, kutokana na kipa huyo wa Bayern Munich kuwa nje kwa majeruhi.

Lakini Neuer aliharakishwa kurejeshwa kwenye kikosi cha taifa kilichofanya vibaya kwenye faiunali za Kombe la Diunia na tangu wakati huo nahodha huyo wa Ujerumani amekuwa ni kipa nambari moja na asiye na mpinzani.

Ter Stegen amekiri kuwa kutokuwa na furaha wiki iiyopita na hali yakemya baadaye kwenye timu ya taifa chini ya Low sasa kuko mashakani.